Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi


Na EmanuelMadafa,Mbeya
Matukio na   makosa ya usalama barabarani katika Mkoa wa Mbeya imetajwa kupungua kwa kiwango cha asilimia 15 katika kipindi cha mwezi Januar hada machi mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi akizungumza jijini Mbeya amesema kuwa  jumla ya makosa na matukio yote yaliyoripotiwa katika kipindi cha Jan – Machi, 2014 yakiwemo makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishaji ni 12,250 wakati kipindi kama hicho Jan-Machi, 2013 yaliripotiwa makosa 14,375 hivyo kuna pungufu ya makosa 2,125 sawa na asilimia 15.

Amesema Matukio ya ajali yaliyoripotiwa kwa kipindi cha JanMachi, 2014 yalikuwa 98 wakati kipindi cha Jan- Machi, 2013 yalikuwa 156  hivyo kufanya kuwepo kwa na upungufu wa matukio 58 sawa na asilimia 37.

Msangi ameabainisha kuwa Matukio ya ajali za vifo yaliyoripotiwa Jan – Machi,  2014 yalikuwa 58 wakati kipindi cha Jan-Machi, 2013  yaliripotiwa matukio 65  hivyo kuna pungufu ya matukio 7 sawa na asilimia 11.

Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi amesema Watu waliokufa kipindi cha Jan-Machi, 2014 walikuwa 61 wakati Jan –Machi, 2013 walikuwa 81 hivyo kuna pungufu ya watu 20, sawa na asilimia 7 huku Watu waliojeruhiwa kipindi cha Jan – Machi,   2014 wakiwa  104 wakati Jan – Machi, 2013 walikuwa ni  91 hivyo kufanya kuwepo kwa na ongezeko la watu 13,  sawa na asilimia 14.

Pia Katika kipindi cha Jan – Machi, 2014,  jumla ya makosa 12,422  ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishwaji yalitozwa faini sawa na tozo la Tshs 332,790,000/=  ikilinganishwa na tozo la Tshs 365,400,000/=  iliyokusanywa katika kipindi Jan – Machi, 2013  kutokana na makosa 14,219, hivyo kuna pungufu la kiasi cha Tshs 32,610,000/=  sawa na  asilimia9.



MATUKIO YA USALAMA BARABARANI KWA KIPINDI CHA JAN-MACHI,  2014 NA JAN – MACHI, 2013.asilimia 9.


MATUKIO
12,250
14,375
-2,125
-15
MATUKIO YA AJALI
98
156
-58
-37
AJALI ZA VIFO
58
65
-7
-11
WALIOKUFA
61
81
-20
-7
WALIOJERUHIWA.
104
91
+13
+14
AJALI ZA MAJERUHI
40
91
-51
-56
MAKOSA YA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA USAFIRISHAJI
12,422
14,219
-1,797
-13
 TOZO [NOTIFICATION]
332,790,000/=
365,400,000/=
-32,610,000/=
-9

 

Mwisho.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top