Ezekiel King Mwenye shati la blue akiteta jambo na nduguze kabla ya kutolewa hukumu.picha na Rashid Mkwinda wa Fasihi Midia |
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mbeya, imemuhukumu kwenda
jela miaka saba, Ezekiel King (52) Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Itiji
(Chadema) Jijini hapa na mwenzake Anthon Kavuruge(53) kwa kosa la shambulio la
kudhuru mwili.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya
Mkoa wa Mbeya Maria Batulaine alisema kuwa washitakiwa hao kwa pamoja
walishtakiwa kwa kosa la kumdhuru mkazi wa Itiji Nicholaus Mwakasinga kwa
kumpiga na kumjeruhi kichwani na mkononi.
Amesema kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo Octoba 4, 2013 wakiwa katika kilabu cha pombe kilichopo eneo la Itiji ikiwa ni kinyume cha sheria namba 225 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Awali akisoma maelezo ya uchambuzi
wake Hakimu Batulaine amesema, mahakama imechambua na kuthibitisha ya kwamba
washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo licha ya kujaribu kuidanganya
mahakama.
Amesema,pia ushahidi wa upande wa
mashitaka kutoka hospitali uliweza kuthibitisha majeraha ya vidonda
kwenye mwili wa Mwakasinga huku ukiweka bayana ya kwamba shahidi namba
moja upande wa mashitaka hakuwa na matatizo ya akili kama ilivyoelezwa na
washitakiwa.
Aidha, kabla ya kutoa hukumu hiyo, Hakimu
Batulane alitoa nafasi ya kujitetea kwa washitakiwa ambao wote kwa pamoja
waliiomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwani familia zao zinawategemea.
Akitoa hukumu hiyo hakimu Batulane,
amesema kuwa mahakama hiyo i imepitia ushahidi wa pande zote mbili na
kwamba umeridhika pasipo kuacha mashaka hivyo kuwahukumu kwenda jela
washitakiwa miaka sabana kwamba rufaa ipo wazi.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mwambigija alisema uongozi umepokea
hukumu hiyo kwa mshangao mkubwa.
Aidha, amesema tayari uongozi umekutana na
kwamba taratibu za kuwasiliana na mwanasheria wa chama zinafanika ikiwa
na kuangalia uwezekano wa kukata Rufaa kabla ya siku 30 kumalizika.
Mwisho.
Post a Comment