Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MKURUGENZI wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameshindwa kumzika baba mdogo wa mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Blandina Chagula, Clement Kiyenze Chagula.
Mzee huyo alifariki katika Hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya presha na figo yaliyokuwa yakimsumbua na kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo wasanii mbalimbali wa filamu nchini walishiriki akiwemo Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Alipoulizwa Ray kwa nini hakuhudhuria mazishi hayo, alisema:
“Ukweli ni kwamba mimi sipo Dar. Ndiyo maana sijaonekana huko kwenye mazishi, nipo Mwanza katika shughuli zangu za kikazi, tuko pamoja lakini,” alisema Ray ingawa wachungzi wa mambo wanasema kuwa alikuwepo mjini ila ni kutokana na sababu binafsi zao kati yake na Johari ndo maana hakutaka kwenda huku chuchu hans akidaiwa kuhusika.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top