Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Na EmanuelMadafa,Mbeya
ALIYEKUWA Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya  Antony Mwakasungura amedaiwa kuvunja ofisi ya chama hicho Wilayani humo kwa lengo la kile kilichodaiwa kutaka kuiba nyaraka mbalimbali za chama.

Tukio hilo limetokea mwanzoni mwa wiki hii katika ofisi za chama hicho ambapo inaelezwa kuwa alivunja mlango na kuingia ndani na kudai kuwa alikuwa akichukua nyaraka zake binafsi.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho Award Kalonga amesema kuwa Katibu huyo alikuwa akikataa kukabidhi ofisi kwa  uongozi mpya pamoja na kuitwa kwenye vikao vitatu mfululizo kwa ajili ya kufanya makabidhiano na uongozi mpya.

Amefafanua kuwa mara baada ya kuingia ndani alianza kupekua baadhi ya mafaili ya ofisi na mengine kuyachana hali ambayo ilizusha tafrani kiasi cha kusababisha vurugu.

Amesema kuwa wakati wa tafrani hiyo kiongozi huyo wa zamani alikuwa akitoa maneno ya kejeli na kutamba kuwa hawawezi kumfanya chochote.

Hata hivyo mara baada ya kutokea vurumai hiyo kiongozi huyo alifanikiwa kuwakimbia viongozi hao na kutokomea kusikojuliana.


Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa jalada la kesi hiyo linashughulikiwa kwa ajili ya kufikishwa kwa mwanasheria ili kufikishwa mahakamani.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top