Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mbunge wa jimbo la Songwe Mheshimiwa PhilpMulugo akipiga magoti mbele ya waziri Mkuu Mizengo Pinda katika Mkutano wa Hadharauliofanyika katika kijiji cha Mbuyuni Kata ya Gua Wilayani Chunya Mkoani mbeya.



Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mbunge wa Jimbo la Songwe Mheshimiwa PhilIp Mulogo ameduwaza wananchi na wapiga kura wake  wa jimbo lake la songwe  kwa kitendo  chake cha kupiga magoti mbele ya waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa lengo la kumshinikiza waziri huyo kutoa tamko juu ya lini barabara ya Mbalizi chunya itakamilika kwa kuwekewa lami.

Hatua hiyo ilikuja katika Mkutano wa hadhara uliofanyika  katika kijiji cha Mbuyuni Kata ya Gua jimbo la Songwe ambapo mbunge alitakiwa kutoa neno la shukrani na kusalimia wananchi  mara baada ya waziri mkuu kudhuru katika halmashauri hiyo ya chunya ikiwa ni sehemu yake ya ziara iliyolenga kutembelea shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazotekelezwa na serikali pamoja na washirika wa maendeleo katika mkoa wa mbeya.

 Mbunge huyo mara baada ya kutoa shukrani zake kwa Waziri Mkuu ghafla alipiga magoti na kutoa maneno ya huruma kwa kumtaka Waziri Mkuu Pinda kutoa tamko kwa wananchi  juu ya lini barabara ya Mbalizi Mkwajuni  itakamilika kwa wakati na kuondoa kero kwa wananchi wa jimbo lake hali ambayo iliibua mshangao mkubwa kwa wananchi na wapiga kura wake.

Akiongea mara baada ya kupiga magoti huku akimtazama Mheshimiwa  Pinda alisema kuwa amekuwa na mtihani mkubwa  kwa wananchi wake kuhusiana na kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo imekuwa ikizungumzwa mara kwa mara na serikali kuwa ipo katika mikakakati ya kujengwa.
Amesema kero kubwa waliyo nayo kwa sasa wananchi wa jimbo hilo ni ubovu wa barabara hiyo kwani ndio kiungo kikubwa cha kusukuma maendeleo katika jimbo lake la Songwe .

Pamoja na kuibua hoja hiyo Pia mheshimiwa Mulugo  alimuomba Mheshimiwa waziri Mkuu kulipa nguvu za kutosha suala la uanzishwaji wa Wilaya katika jimbo hilo ambalo makao makuu yake yamependekezwa kuwa Mkwajuni

Akizungumzia  hoja hizo za Mbunge kwa kuanza na suala la barabara Mheshimiwa Pinda alisema tayari hatua za  awali zimekwisha fanyika kwa kwa kuufanyika upembuzi yakinifu hivyo amewataka wananchi wa jimbo la songwe pamoja na mbunge huyo kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea na mchakato huo.

Amesema pamoja na juhudi hizo pia atajalibu kuzunguzma na Waziri Magufuli ili kufahamu kwa kina juu ya kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo ya Chunya Mbalizi yenye kilomita 60 .

Kuhusiana na ombila kuanzishwa kwa Wilaya katika jimbo hilo Waziri Mkuu Pinda amesema tayari wamekwisha pokea ombi ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) cha Mkoa wa Mbeya yanayopendekeza mkoa huo ugawanywe na kupata mikoa miwili ya Mbeya na Songwe.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali imeridhia maombi hayo kutokana na ukubwa wa mkoa huo ambao una kilometa za mraba 63,000 ambapo nusu yake ni Wilaya ya Cunya.
 Amesema kamati hiyo imeshauri mkoa huo ugawanywe katika wilaya nne nne ambapo mkoa mpya wa Songwe utakuwa na wilaya za Ileje, Momba, Mbozi na Chunya.

 Alisema katika kikao hicho ilikubaliwa kwamba makao makuu ya wilaya mpya ya Songwe yatakuwa Mkwajuni .

. “Nimekubali maombi haya kwa sababu yatapunguza gharama za uendeshaji, na kama itashindikana kupata wilaya mpya basi itabidi tuwape Halmashauri ya Songwe,” alisema.
 Mkoa wa Mbeya una wilaya nane ambazo zimegawanyika katika tarafa 27, kata 262, vijiji 842 na mitaa 252. Idadi ya wakazi kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni 2,707,410.

Mwisho
 JAMIIMOJABLOG

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top