CECAFA leaders Nicholas musomnye (l), leodegar tenga and
Jamal malinzi at CECAFA Press conference in Dar yesterday….
|
Rais wa Baraza
la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga
leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza
kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar
es salaam.
Akiongea na
waandishi wa habari leo katika ofisi za TFF zilizopo Karume, Tenga
ameishukuru serikali ya Tanzania na TFF kwa kukubali kuwa wenyeji wa
michuano hiyo mikubwa, vyombo vya habari na wapenzi wa mpira wa miguu
nchini kwa sapoti yao na kuipokea kwa mikono miwili michuano hiyo.
Lengo la
CECAFA ni kuona vilabu vya ukanda huu vinapata nafasi ya kucheza michezo
mingi na kujiandaa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe
la Shirikisho barani Afrika.
Naye Rais wa
TFF, Jamal Malinzi amewashukuru CECFA kwa kuipa Tanzania uenyeji huo na
kuahidi TFF itahakikisha michuano hiyo inafanya nchini katika hali ya
amani na usalama toka mwanzo mpaka mwisho wa michuano hiyo.
Timu
zilizothibtisha kushiriki michuano hiyo ni Yanga, Azam (Tanzania), APR
(Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar),
Khartoum-N (Sudan), Al Shandy (Sudan) LLB AFC (Burundi), Heegan FC
(Somalia), Malakia (Sudani Kusini), Adama City (Ethipia) na KCCA
(Uganda).
Wakati huo
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ametangza ratiba ya michuano ya
Kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es
salaam ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa CECAFA.
Mechi ya
ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
itashuhudia wenyeji Yanga SC wakicheza na Gor Mahia ya Kenya, huku APR
ya Rwanda ikicheza na Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua
dimba na Telecom ya Somalia.
Ratiba ya
michuano hiyo imeziweka timu hizo katika makundi matatu ambapo kundi A
lina timu za: Yanga (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djbiout),
KMKM (Zanzibar) na Khartoum-N (Sudan)
Kundi B: APR
(Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB AFC (Burundi) na Heegan FC (Somalia),
Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City
(Ethiopia) na KCCA (Uganda)
Timu tatu
zitakazoshika nafasi ya juu kutoka kundi A, timu mbili za juu kutoka
kundi B & C, na mshindi mwenye wastani mzuri kutoka kundi B & C
zitaingia katika hatua ya robo fainali.
BENDERA AIPONGEZA TFF
Mkuu wa mkoa
wa Manyara Dokta, Joel Bendera ameipongezs TFF kwa kuandaa mashindano ya
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13), na maandalizi
ya timu hiyo kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika za vijana
chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.
Bendera
amesema hiyo ndiyo njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio pia
amepongeza juhudi za Chama cha Soka mkoa wa Manyara na TFF kwa kuandaa
kozi za makocha na waamuzi, akisema huo ndiyo uwekezaji mkubwa katika
maendeleo ya soka mkoani Manyara.
Aidha aliwaasa
makocha kutumia mbinu za kisasa za ufundishaji soka walizozipata kwenda
kuendeleza vipaji vya wachezaji watakaowafundisha.
Pia Bendera
amewahakikishia wakazi wa Manyara atahakikisha wanaandaa vipaji
vitakvyowawezesha kuwa na timu bora itakayowakilisha mkoa wa Manyara.
ACCREDITATION FOR ALL AFRICAN GAMES:
Shirikisho
la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limetangza kufunguliwa kwa maombi
ya vitambulilsho kwa wandishi wa habari kwenye fainali za michezo ya
Afrika zitakazofanyika mwezi Septemba mwaka huu nchini Congo-
Brazaville.
Waandishi
wa habari wanaotajiwa kwenda kufanya kazi kwenye michuano hiyo
wanaombwa kufanya maombi ya vitambulisho (Accrediatation) kuanzia Juni
29 mpaka Julai 7 mwaka huu.
Link ya kufanya maombi hayo ni @CAF_Online
Accreditation for African Games Congo 2015 draw
Post a Comment