Na Kibada Ernest Kibada-Mbeya.
Imeelezwa
kuwa Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini inakabiliwa na utapiamlo mkubwa pamoja na kuwa inaongoza kwa uzalishaji
wa chakula nchini lakini wakazi wake walio wengi hususani watoto na baadhi ya
watu wazima wanakabiliwa na tatizo la utapia mlo ni mkubwa sana.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa majuuisho baada ya
kutembelea maonesho ya Nanenane alipotembelea Banda la Halmashauri ya wilaya
ya Mpanda Mkoa wa Katavi na kukutana waoneshaji pamoja na wajasiliamali
wanaosindika unga wa lishe.
Amesema kuwa
Mikoa na Halmashauri zote za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini zinatakiwa kufanya
tathimini ya utapiamlo na kuhakikisha tatizo hilo linakwisha katika kanda hii.
Amesisitiza
kuwa itolewe elimu ya kutosha kwa akina
mama namna ya kuepukana na suala la utapiamlo kwa watoto,na akina mama wanapokuwa katika hali ya ujauzito
siku 90,ukuzi mzuri wa mtoto anajengwa kwa lishe bora siku 1000 tangu kutungwa
kwa mimba siku 1000 hapo ndipo muda mzuri wa kujenga akili ya mtoto.
Amebainisha kuwa uwezo mzuri wa kufikiriunatokana na jinsi
unavyweza kumtunza mtoto tangu kutungwa kwa mimba akiwa tumboni mwa mama na
ukikosea katika kipindi hicho bila kumpatia lishe bora mama mjamzito unaweza
kuzaa watoto ambao wakati mwingine ni mazezeta,wenye mtindio wa ubongo kutokana
na kukosa lishe bora na utapiamlo unakuwa mkubwa miongoni mwa jamii.
Akizungumzia
kuhusu soko la bidhaa za wajasiliamali zinazozalishwa katika Mikoa ya Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini zinatakiwa ziwe na soko la kudumu na lenye uhakika,baada
ya kuwa na soko la uhakika uzalishaji wa bidhaa uongezeke na ubora
wa bidhaa pia uongezeke.
Aidha
akasisitiza kuwa wajasiliamali wafanyiwe ufuatiliaji wa bidhaa wanazoziuza na
kununua kutoka nchi za jirani jinsi zinavyotengenezwa ili nao waweze
kuzitengeneze bila kutegemea kutoka nje ya nchi.
Mkuu huyo wa
Mkoa akasisitiza wataalamu kuwasaidia wajasiliamali kupata vifungashio vya
bidhaa vyenye u bora katika utunzaji wa bidhaa.
Amefurahishwa
na bidha kutoka Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi jinsi bidhaa hizo
zilizofungashwa akashauri wataalam wa kilimo kuwatafutia soko la bidhaa zao
namna ya kufungasha bidhaa hizo kwa ubora unaotakiwa.
Pia akiwa
kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkuu huyo wa Mkoa alizindua
Kalenda ya Mkulima ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Mwisho.
Post a Comment