·
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BOKA
KASULA (50) MKAZI WA SONYANGA
AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI ALP 3965 AINA YA SCANIA BASI MALI YA KAMPUNI YA WADACHOVU
ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ERNEST
CLEMENCE (42) MKAZI WA ILOMBA IKITOKEA DSM KUELEKEA MALAWI.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 02.09.2015
MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA SONYANGA, KATA YA MAHONGOLE, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA
MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.
MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA IGURUSI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO
KASI, DEREVA AMEKAMATWA. UPELELEZI UNAENDELEA.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MPANDA BAISKELI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA THADEO MWASHILANGA (21) MKAZI WA ICHENJEZYA WILAYA YA MBOZI AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUGONGWA NA GARI ISIYOFAHAMIKA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 02.09.2015
MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA ILOLO, KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA
WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.
MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO NI MWENDO KASI NA
DEREVA ALIKIMBIA NA GARI BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
TAARIFA
ZA MISAKO:
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AIDAN
JOHN (32) MKAZI WA UYOLE-MBEYA ANASHIKILIWA
NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 25.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA
MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI
CHA KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA
YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
KATIKA
OPERESHENI ILIYOFANYIKA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO ENEO LA MATENKI,
KATA YA NJISI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA, MTU MMOJA
AITWAYE MWINUKA NGONYA (30) MKAZI WA MATENKI AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU
NCHINI AINA YA RIDDER BOKSI 08 NA CHARGER BOKSI 2.
AIDHA
KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA
WILAYANI CHUNYA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA
YA SAA 15:30 JIONI HUKO KATIKA
KIJIJI CHA MATUNDASI [B], KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA GEORGE SAWELA (44) MKAZI WA MATUNDASI NA GILBERT
SILWANI (43) MKAZI WA MATUNDASI WAKIWA NA MILIPUKO BARUTI 136 PINI ZA MILIPUKO 35,
COTEX MITA 70 NA DOTNETOR 2 BILA
KIBALI.
TARATIBU
ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA
ZINAENDELEA.
Imetolewa
na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment