Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Katikati)akizungumza na viongozi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya,kulia Mkurugenzi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya Jovent Rushaka na Meneja Utawala na fedha Bakali Ally kushoto katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya ,June 28 -2016.

Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakimsikiliza kwa makini Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo June 28 mwaka huu.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Amosi Makalla akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika kwa engo la kujitabulisha
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (katikati)akiwa pamoja na viongozi waandamizi wa benki kuu Tanzania (BOT) tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo June 28 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki kuu Tanzania (BOT)Tawi la Mbeya ,

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameitaka benki kuu kuendeleza jitihada za Kudhibiti mfumuko wa bei, noti BANDIA NA ubadilishaji Fedha kiholela ni vitu hatari kwa uchumi
Hayo aneyasema leo alipokutana na viongozi na wafanyakazi wa benki kuu kanda ya kusini katika ziara zake za kikazi
Amesema kwa ajili ya kuwa na uchumi mzuri na kuwa na thamani ya fedha kiwango kinachoruhusiwa ni mfumuko wa tarakimu moja hivyo mfumuko wa bei Tanzania bado ni wa tarakimu moja na lazima tuendelee kudhibiti na lazima tufanye jitihada za kujitosheleza kwa Chakula na malighafi ya viwanda vyetu na uuzaji zaidi bidhaa nje kuliko kuagiza
Aidha emesema endapo ubadilishaji wa fedha za kigeni hautadhibitiwa na uchapushaji noti BANDIA utaongeza mzunguko wa fedha usio rasmi na ni hatari kwa uchumi na usalama
Amewataka benki kuu kitengo cha uchumi kufanya utafiti nini kufanyike kwa hali ya sasa baadhi ya wafanyabiashara kununua Mazao ya mkulima yakiwa shambani na kumpangia bei mkulima na hata kama bei itapanda bado mkulima analipwa bei ya awali ya makubaliano amesisitiza jambo hilo halikubaliki kwani linamdidimiza mkulima
Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top