Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiongea
na wadau wa michezo katika ufunguzi wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) ulioanzishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) leo Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi akisoma
risala wakati wa ufunguzi wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) ulioanzishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu lengo ikiwa ni
kubuni vyanzo mbalimbali vya rasilimali ili kuwezesha shirikisho hilo
katika kutekeleza kazi zake.
Mkuu wa Kitengo cha Ufundi wa Maendeleo ya Soka nchini Bw. Kim Poulsen
akiongea na wadau wa michezo katika uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia)
akijadiliana jambo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) Bw.Jamal Malinzi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) leo Jijini .
Wajumbe
wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) kushoto ni
Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe, Katikati ni Mkurugenzi wa
Mawasiliano Airtel Beatrice Singano na kulia ni Meneja Mwandamizi wa
Benki ya NBC Salmi Rupia.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
(kulia) akimkabidhi nyaraka za Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) kwa Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe (kushoto),
ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo ,katikati ni Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi.Leo Jijini dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia)
akimkabidhi nyaraka za Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu
(FDF) kwa Meneja Mwandamizi wa Benki ya NBC Salmi Rupia(kushoto),
katikati ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Bw.Jamal Malinzi.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) mara baada ya kuuzindua leo Jijini Dar es Salaam
.(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM).
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Serikali
imeunga mkono uwanzishwaji wa Bodi ya Maendeleo ya Mpira wa Miguu (TDF)
wenye lengo la kuratibu vyanzo mbalimbali vya mapato ili kutekeleza
maendeleo ya mpira nchini ikiwemo kukuza vipaji vya michezo kwa vijana
wa kike na wa kiume.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye alipozindua Bodi hiyo iliyo chini ya uratibu wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania leo Jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka
wadau wa michezo,wananchi na sekta binafsi kuunga mkono jitihada hizo.
“Jambo hili ni jema sana katika sekta ya michezo nchini hivyo ni
jukumu letu sote kuhakikisha tunaunga mkono juhudi hizi zenye lengo la
kuleta matokeo chanya katika sekta hii muhimu mfano mzuri ni vijana wetu
wa Serengeti Boys wameshatuonyesha kuwa tunaweza kufika mbali” alisema
Waziri Nnauye.
Aidha,
aliitaka Bodi hiyo kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili
kuhakikisha mfuko huu unakua na hivyo kuwezesha utendaji fanisi wa
kukuza vipaji vya michezo wa kike na wa kiume na kwa wale watakaokiuka
miiko ya kazi uongozi usisite kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yao.
Naye,
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi
alieleza kuwa lengo la kuunda mfuko huo ni kusaidi katika kuendesha
shughuli za Shirikisho ambapo kutakuwa na utaratibu maalum wa kuomba
fedha kutoka katika mfuko huo.
“Kiutaratibu
Sekretrarieti ya TFF ikiwa na mahitaji itakuwa inatuma maombi kwenda
bodi na pale bodi inaporijiridhisha na uhalali wa maombi hayo itatoa
ruhusa kwa Shirikisho kuendelea na utaratibu wa kupatiwa fedha “alisema
Bw.Malinzi.
Bw.
Malinzi aliongeza kwa kuahidi kuwa TFF itahakikisha Tanzania inang’ara
kimataifa katika mpira wa miguu kwa kufuzu kucheza fainali za kombe la
Dunia mwaka 2026 kwa upande wa wanaume (Taifa Stars) na kwa upande wa
wanawake (Twiga Stars) 2019.
Akiongea
kuhusu kuwekeza katika mpira wa vijana Bw. Malinzi alisema kuwa Msingi
mkubwa wa mafanikio ya timu za taifa duniani kote ni kuwekeza katika
mpira wa vijana ili kuhakikisha wanafundishwa mpira kwa kiwango cha
kimataifa katika umri mdogo utakaowasaidia kuwa imara.
Bodi
ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ulirasimishwa rasmi
katika Mkutano Mkuu wa TFF wa mwaka 2015 hivyo mfuko huo upo katika
katiba ya TFF huku jukumu lake kubwa ikiwa ni kubuni vyanzo mbalimbali
vya mapato ambavyo vitasaidia Shirikisho hilo katika kutekeleza kazi
zake mbalimbali za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Post a Comment