Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kundi la Uigizaji wa Filamu ‘Bongo Movie Shinyanga’ limempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua anazozichukua katika kulinda rasilimali za nchi hususani madini ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga, Juma Songoro amesema rais Magufuli anapaswa kuungwa mkono na wananchi wote wa Tanzania na wazalendo wote. "Wasanii wa filamu mkoa wa Shinyanga tunampongeza sana rais Magufuli kwa hatua anazozichukua kulinda nidhamu na rasilimali za nchi,tunamuombea kila la heri atufikishe tunapopatarajia,tumeandaa filamu hii kama zawadi yetu kwake na na watanzania wote",amesema Songoro.
Katika kufikisha pongezi hizo,Bongo Movie Shinyanga wameandaa Filamu fupi inaitwa 'Tanganyika Karne ya 18' inayoonesha  jinsi nchi za nje zinavyoiba madini ya Tanzania.
TUMIKA DAKIKA ZAKO 3 TU KUTAZAMA FILAMU HII HAPA CHINI

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top