Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
SINGIDA
United inaingia kambini kesho kwa ajili kujiandaa na msimu mpya wa ligi
kuu Vodacom huku ikizitahadharisha timu za Simba na Yanga kuwa hawana
undugu nao na kama kuna wanaodhani hivyo wanaota ndoto za mchana kwani
wataujua ukweli baada ya kuanza msimu mpya wa ligi utaoanza mwezi
Agosti.
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja wa klabu hiyo Festo Sanga mbele ya Waandishi
wa Habari na kuondoa utata ulioanza kujitokeza kuhusu baadhi ya viongozi
kuwa na mapenzi na timu hizo kongwe nchini.
Kumekuwa
na dhana kuwa Singida inaweza kuwa undugu na karibu na Yanga kwakua
kiongozi wake mkuu Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, kocha mkuu
wa timu hiyo Mholanzi Hans Pluijm na msaidizi wake Fred Minziro wote
wakiwa ni wapenzi wakubwa wa mabingwa hao wa ligi kuu msimu uliopita.
"Inawezekana
kuna viongozi wana mapenzi na timu za Simba na Yanga ila Singida United
haitambui hilo, na mkitaka kuamini kauli yangu subirini ligi ianze
ndiyo mtaona kitakacho tokea," alisema Sanga.
Singida
itaingia kambini kesho jijini Mwanza kwa ajili ya kambi kujiandaa na
msimu mpya wa ligi mwezi ujao ambapo imepanga kutafuta mechi za kirafiki
kutoka nchi za Kenya, Uganda na Rwanda.
Wakati
huo huo Sanga alisema wamefanikiwa kununua basi la klabu hiyo aina ya
Dragon lenye thamani ya shilingi milioni 350 watakalo litumia kusafiri
sehemu mbalimbali kuanzia sasa.
" Tumefanikiwa kununua basi kwa ajili ya safari zetu za timu ndani na nje ya nchi kuanzia sasa," alisema Sanga.a
Muonekano wa gari la Singida United linaloratajiwa kutumiwa na wachezaji wa timu hiyo katika msimu mpya wa ligi kuu.
Meneja
wa klabu ya Singida United Festo Sanga akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa kulitambulisha basi lao jipya litakalotumika kwa safari
za ndani za timu ya Singida United.
Post a Comment