Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na wajumbe wa kamati ya siasa mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017. Picha zote Na Mathias Canal

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017.
Na Mathias Canal, Mbeya

Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya kimemshukuru na kumpongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kumteua Mhe Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo kuhudumu katika nafasi hiyo katika serikali ya awamu ya tano.

Pongezi hizo pamoja na shukrani zimetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya siasa wakati akitoa taarifa ya chama hicho Ofisini kwake Mara baada ya Naibu Waziri kuzuru katika Ofisi hizo akiwa ziarani Mkoani Mbeya.

Nkambaku alisema kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi muhimu kwani Mhe Mwanjelwa ni mchapakazi na msaada mkubwa kwa chama hicho hivyo uteuzi huo umeonyesha Imani kwa Chama Cha Mapinduzi na Wananchi wa Mkoa mzima wa Mbeya.

Aidha alimsihi Kutenda haki na kufanya kazi kwa bidii huku CCM ikiahidi kutoa ushirikiano mwema Kwa Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Mbeya.

Akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kwenye Ukumbi wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa aliwasihi makada hao Kutofanya kazi za Chama kwa Mazoea badala yake kufanya kazi kwa weledi ili kuwasaidia wanachama na wasiokuwa wanachama wa CCM katika shughuli za maendeleo.

Naibu Waziri Huyo ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC) amejivunia malezi bora na muhimu aliyoyapata ndani ya Chama Cha Mapinduzi huku akiwasihi viongozi kuongeza bidii katika kumsaidia Rais Magufuli kutimiza ndoto ya Tanzania Mpya kwa manufaa ya watanzania katika kuwaletea maendeleo.

MWISHO.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top