Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanamke mmoja amefariki akipiga picha aina ya Selfie na rafikiye katika barabara ya treni nchini Thailand.Rafikiye alisema kuwa walikuwa wamekunywa pombe na kuamua kujipiga picha hiyo na treni lakini hawakuona treni nyengine iliokuwa ikija kutoka barabara nyengine ya treni, kwa mujibu wa polisi.
Miguu yake ilikatika na kufariki hospitalini ambako alikuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi.
Rafikiye wa kiume alipata majeraha mabaya.
Idadi ya watu wanaofariki wakipiga selfie katika maeneo hatari inaongezeka.
Kisa hicho kilitokea siku ya Alhamisi asubuhi katika kituo cha treni cha Samsen mjini Bangkok, kulingana na maafisa wa polisi wa Wissanusak Seub akiongezea kwamba maafisa walikuwa wakichunguza kilichotokea

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top