Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii
WAZIRI
wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango amesema Tanzania inakadiriwa kuwa
na idadi ya watu wapatao milioni 54.2 huku asilimia 50 wakiwa ni wa
umri chini ya miaka 18.
Pia
Dk.Mpango amewakumbusha wadau wote was ndani na nje ya nchi kuwa takwimu
za idadi ya watu kwa nchi ya Tanzania ni hizo ambazo amezitangaza leo
na si vinginevyo.
.
Hivyo
amepiga marufuku kwa shirika lolote kufanya makadirio ya idadi ya watu
wa Tanzania na kuchapisha matokeo hayo bila kushirikisha Ofisi ya Taiga
ya Takwimu na atakayebainika kufanya hivyo watamchukulia hatua kali za
kisheria.
Dk.Mpango
amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazondua taarifa ya
makisio ya idadi ya watu Tanzania amvapo amesema kwa makadirio
yaliyotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
Na
kuzingatia viwango vya uzazi na vifo kwa takwimu za mwaka 2016, idadi ya
watu Tanzania sasa ni milioni 52.6 ambapo Tanzania Bara ni watu milioni
52.6 na Tanzania Bara watu milioni 1.6 kwa mwaka 2018.Dk.Mpango
amesema idadi hiyo inakadiriwa kufikia watu milioni 59.4 mwaka 2021 na
ifikapo mwaka 2030 idadi ya watu itafikia milioni 77.5.
Amefafanua
kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012
inakadiriwa kuwa kila mwaka kuna ongezeko la wastani watu wapatao
milioni 1.6 hapa nchini.Dk.Mpango
amesema ongezeko hill linatokana na idadi kubwa vya vizazi vipatavyo
milioni 2.0 ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo ambavyo ni takribani
400,000 kwa mwaka.
"Utafiti
wa mama na mtoto wa mwaka 2015/16 unaonesha kwamba mwanamke wa
kitanzania atazaa watoto watano katika maisha yake yote ya uzazi .
" Hata
hivyo kiwango cha uzazi kilipungua kutoka wastani wa watoto 7 mwaka
1978 had I wastani wa watoto watano mwaka 2016.Baadhi ya sababu za juu
cha uzazi ni kiwango kikubwa cha vifo vya watoto,familia kupendelea kuwa
na watoto wengi,umasikini,mila,imani za kidini na matumizi madogo ya
uzazi wa Mpango,"amesema.
Ameongeza
matokeo yake ni kuwa na idadi ya watu hapa nchini imeendelea kuongezeka
na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya sita katika Bara la Afrika kwa kuwa
na idadi kubwa ya watu baada ya Nigeria, Ethiopia, DRC na Misri.
Amesema
kwa mtazamo wake wingi au au uchache wa idadi ya watu sio tatizo bali
tatizo ni pale ambapo kasi ya ongezeko la idadi hiyo inazidi kasi ya
ukuaji wa uchumi na hivyo kulifanya Taifa kushindwa kumudu ipasavyo
mahitaji ya wananchi.
Dk.Mpango
amesema kasi ya ongezeko la idadi ya watu pia inaleta changamoto ya
idadi kubwa ya watoto na vijana ."Kwa mfano takwimu nilizozizindua leo
zinaonesha asilimia 50 ya watu wote nchini ni watoto wenye umri chini ya
miaka 18.
"Asilimia
hii kubwa ya watoto katika nchi zinazoendelea inatokana na mabadiliko
ya kidemografia kutoka viwango vya juu vya vifo lakini wakati huo
viwango vya uzazi vibaki juu," amesema.
Ameongeza
asilimia kubwa ya watoto ni changamoto kwa maendeleo ya nchi yoyote
duniani kwa vile kundi hilo lina mahitaji ya kipekee ambayo lazima
yatimizwe na Serikali na jamii kwa ujumla wake.Dk.Mpango amesema mojawapo ya changamoto hizo ni kiwango cha juu cha utegemezi kinachotokana na idadi kubwa ya watoto.
Amesema
kwa mfano kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kiwango
cha utegemezi kiumri ni asilimia 92 ikilinganishwa na wastani wa
asilimia 40 kwa nchi zinazoendelea.Hiyo
ikiwa na maana kuwa kwa Tanzania kila watu 100 wenye umri wa miaka 15
hadi 64 wanategemewa na watu 92 wenye umri chini ya miaka 15 wenye umri
zaidi ya miaka 65.
Dk.Mpango
amesema ili kukabiliana na changamoto hizo za ongezeko la idadi ya watu
,Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikiwa pamoja na kutunga na
kutekeleza sera ya idadi ya watu ya mwaka 1992 na ilifanyiwa
marekebisho mwaka 2006.
Amesema
lengo la Sera hiyo ni kutoa ni kutoa miongozo ya kushughulikia masuala
ya idadi ya watu.Kwa kutambua kuwa kuna mahusiano baina ya mwenendo wa
idadi na ubora wa maisha ya wananchi kwa upande mmoja na ulinzi wa
mazingira.
Post a Comment