Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu na kuwapa pole wakazi wa Mbalizi wakati akiwasili mkoani Mbeya tayari kwa ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu na kuwapa pole wakazi wa Mbalizi wakati akiwasili mkoani Mbeya tayari kwa ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Na EmanuelMadafa,Mbeya
MAKAMU wa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu, amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Mbeya, kwamba serikali imejipanga kutekeleza na kutatua changamoto muhimu za kimaendeleo, ikiwemo ya miundombinu ya barabara.
Makamu wa Rais, ameyasema hayo, leo wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika eneo la Mbalizi Wilayani Mbeya, eneo linalotajwa kuongoza kwa matukio ya ajali za barabarani.
Amesema, katika kulitekeleza hilo, tayari serikali imeshughulikia changamoto ya ujenzi wa barabara ya mchepuko ya kilomita 40 ambayo itasaidia kupunguza au kudhibiti ajali za barabarani zinazotokea kwenye barabara kuu ya Tanzania na Zambia (TAZAMA).
 “Mwaka juzi mlifanya kazi kubwa sana, tumekuja kuwahikikishia kwamba serikali itatekeleza yale yote tuliyo ahidi, nadhani spidi mnaiona,”amesema.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani kwani ndio sialaha ya maendeleo na kuwasisitiza kuchaguai viongozi watakaoendana na kasi ya rais na waioendekeza tama wakati wa uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa.
Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top