Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Na EmanuelMadafa Michuzi Blog -MBEYA.

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mkazi wa kijiji cha Isutu Kata ya Ilongo Wilayani Mbarali Geofrey Emilo kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa  miezi mitano Prince Geofrey  kisha kuufukia mwili wake porini.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Modestusi Chambu, alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashahidi mbalimbali, inadaiwa kuwa mtuhumiwa alimuua mtoto huyo kwa kumnywesha sumu ambayo bado haijafahamika aina yake na kwenda kumfukia porini.

Kwa mujibu wa Kamanda Chambu, alisema tukio hilo limetokea Agosti 28 mwaka huu katika Kijiji cha Isitu porini, Kata ya Chimala, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya
Ambapo baba mzazi huyo alikwenda nyumbani kwa mtalaka wake mke baada ya kutengana na kumchukua mtoto huyo kwa nguvu bila kibali cha mama mzazi wa mtoto.
.

Alisema, Agosti 30, mwaka huu mtuhumiwa alikamatwa na alipohojiwa alikiri kuwa mtoto huyo amemuua na kumtupa porini na katika ufuatiliaji aliwapeleka askari eneo alipokuwa amemfukia marehemu.

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi kwani mtuhumiwa alikuwa anahisi mtoto huyo sio wake amebambikiwa ni wa mwanaume mwingine,”alisema.

Katika tukio lingine polisi Mkoani Mbeya, linawasaka watu wanaodaiwa kufukua kaburi na kisha kuchukua mifupa ya mwili wa marehemu ambaye alikuwa na ulemavu wa ngozi (Albinism).

Tukio hilo limetokea tarehe 30.08.2018 majira ya saa 03:00 usiku huko katika Kijiji cha Ngonga, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa mbeya ambapo kaburi la mtu mmoja aliyekuwa anajulikana kwa jina la Andusamile Mwalwebe (65) Mkazi wa kijiji cha Ngonga ambaye aliyefariki dunia mwaka 2012 kwa maradhi ya kawaida.

Kaimu Kamnada wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Modestusi Chambu, alisema kaburi la mlemavu huyo wa ngozi, lilikutwa limefukuliwa na mtu/watu wasiojulikana na kisha watu hao kuchukua mifupa ya mwili wa mtu huyo ( skeleton) a kwamba kiini cha tukio hilo ni imani za kishirikina.
Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top