Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Meya wa jiji la Mbeya David Mwashilindi akisaini Mkataba kwa ajili ya uboreshaji wa Miundombinu ya barabara katika jiji la Mbeya.
 Na JamiiMojaBlog

HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, leo imeingia mkataba na makandarasi mbalimbali wa ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na madaraja katika Kata 14.

Mkataba huo, umesainiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi huku ukishuhudiwa na baadhi ya madiwani wa Kata husika pamoja na mwanasheria wa halmashauri hiyo Davis Mbembela.

Awali akizungumzia tukio hilo kabla ya kusaini, Meya Mwashilindi amesema, mkatba huo,  unalenga kuboresha miundombinu katika baadhi ya kata katika halmashauri hiyo  ambapo kazi hiyo inataraji kuanza mapema mwezi huu.

Aidha, amesema  kuwa mkataba huo unagharimu kiasi cha shilingi milioni 300 na kwamba kazi kubwa itakayofanyika ni uboreshaji wa barabara na matengenezo ya madaraja katika kata 14 kati ya 36 zilizomo ndani ya Jiji la Mbeya.

“Kampuni zilizoingia mkataba leo ni tano na zote ni makandarasi wa ndani na kubwa zaidi ni wazawa,”amesema.

Pia,  Mwashilindi amewataka makandarasi waliochukua kazi hizo kuhakikisha wanafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa na kwa muda muafaka huku akiwatoa hofu juu ya fedha, kwani bajeti ya matengenezo hayo tayari imeidhinishwa..

Hata hivyo, katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia 100, Mwashilindi amewataka watendaji pamoja na madiwani kuhakikisha wanatembelea na kukagua miradi hiyo, wakati ikiendelea kufanyika na kuachana na tabia ya kusubili mradi ukamilike na kukabidhiwa na ndipo kuanza kubaini kasoro.

“Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi na asilimia kubwa inatokana na kodi za wananchi hivyo ninawaombeni madiwani na watumishi hasa wa idara husika kuhakikisha mnatembelea na kuukagua mradi huu wakati wote wa mchakato, sitapenda kusikia changamoto mara baada ya mradi kukamilika,”amesema.

Mwisho.

Baadhi ya Wakandarasi wa makampuni mbalimbali ya jiji la Mbeya wakisaini mikataba kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara katka baadhi ya kata jijini Mbeya

Baadhi ya Wakandarasi wa makampuni mbalimbali ya jiji la Mbeya wakisaini mikataba kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara katka baadhi ya kata jijini Mbeya hafla ambayo imehudhuriwa pia na baadhi ya madiwani na watendaji wa halmashauri ya jiji katika ofisi ya Meya .

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top