Msanii mkongwe wa
muziki, Mr Nice amesikitishwa na watu ambao wamemzushia kifo katika
mtandao wa kijamii.Mtandao mmoja wa kijamii uliandika taarifa za uongo
kwamba muimbaji huyo amefariki akiwa nchini Tanzania.
Mr Nice ambaye yupo
nchini Kenya amesema alishangaa kuona watu wakimpigiwa simu kwa nyingi
na kuulizwa kuhusu afya yake na alivyofuatilia akagundua kuna mtandao
umeandika taarifa za uongo kwamba amefariki.
Kupitia facebook, Mr Nice aliamua kuandika taarifa hii:
East africa vibes
nawashukuruni sana kwa kunizushia kifo sina la kuwajibu ,,ila mungu
awalipe kadri ya vile mnavyostaili kwa hiki mlichonizushia leo ….mungu
ni wetu sote na hasikilizi amri za binadamu so atakaponihitaji ataniita
kwa mapenzi yake but si nyie east african vibes mnaoweza kuniua wala
yeyote yule chini ya hili jua …kama nyie hamuioni thamani yangu hilo ni
juu yenu kwani huku niliko mimi ni kama lulu na maisha yanaendelea tena
kwa kiwango cha juu kabisa ..hii si mara ya kwanza kunizushia kifo na
mambo mengine ya ajabu ajabu ila all in all mi nipo na bado mtaniona
sana nikiendelea kuwepo ….im total dissapointed kwakweli …mungu awape
stahiki yenu ..THANKS SANA EATV 13/12/2016
Post a Comment