Shughuli zikiendelea |
Karibu mniungisheee akina bibi |
Hivi ndio vyoo vinavyo tumiwa sokoni hapo |
Yaani tunatoa kila siku shilingi miambili 200 kama ushuru kwa kila meza lakini kama unavyoona choo hakifai sijui wahusika kama wanaliona suala hilo amedai mtu huyu. |
Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Itigi |
Amesema pamoja na ubovu wa miundombinu katika soko hilo lakini pia soko hilo halipo rasmi katma masoko mengine licha ya Halmashauri ya jiji kuendelea kuchukua ushuru kwa shilingi miambili kwa kila meza huku akidai kuwa watu wanao fanya biashara katika eneo hilo wanatambua kabisa kuwa soko hilo sio rasmi kwa shughuli za kisoko.
Amesema kwa sasa mipango iliyopo ni kuwatoa watu hao na kuwapeleka eneo jingine ambalo teyari limekwisha tengwa kwa ajili ya shughuli hizo za soko kwani mipango ya halimashauri ni kuwaondoa watu hao na kuweka Kituo cha Afya .
.
Amesema pamoja na kuwepo kwa mipango ya kuboresha hali ya soko hilo laikini pia ametoa lawama kwa wajasilimali hao kwa kudai kuwa hata wao kwa upande wao wanahusika na usafi wa mazingira sokoni hapo licha ya kwamba halimashauri ya jiji kuwa ndio mhusika mkuu wa usafi katika eneo hilo.
Amedai kuwa hata wao pia wanauongozi wao ambao unaweza kuratibu shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira sokoni hapo badala ya kulalamikia mamlaka husika kuwa zimeshindwa kuboresha usafi katika eneo hilo.
Jumla ya wachuuzi 1000 wa mbogamboga na matunda watumia sko hilo ambalo kwa sasa lipo katika hatari ya kutokea kwa magonjwa ya mlipuko hivyo juhudi za haraka zinahitajika ili kuokoa hali hiyo
mwiso.
Post a Comment