Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Ahmed Msangi akifafabua jambo kwa waandishi wa habari jijini mbeya |
Waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza Kamanda Msangi. |
Na Mwandishi wetu,Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amewataka askari Polisi Mkoani humo kuhakikisha wanabadilisha mfumo wa doria ili kupunguza vitendo vya kiharifu pamoja na malalamiko kwa wananchi.
Amesema kwa muda mrefu sasa askari polisi wamekuwa wakifanya doria kwa kupita katika maeneo mbalimbali hasa majira ya usiku huku wakiwa ndani ya magari badala ya kupita kwa wananchi na kujua kero zao.
Kamanda Msangi ametoa wito huo wakati akitoa tathimini ya vitendo vya kihalifu mkoa wa mbeya kwa kipindi cha mwezi januari hadi februari mwaka huu .
Amesema vitendo vya kihalifu pamoja na malalamiko toka kwa wananchi imeilazimisha ofisi yake kubadilisha mfumo huo na kuanza kupita katika maeneo ya karibu na wananchi na kuonana na viongozi wa maneo hayo ili kujua kero zao .
Kamanda Msangi amewataka askari hao kufuata utaribu huo kwani kutasaidia pia kujua vitendo vya kihalifu katika maneo husika na kuzipatia ufumbuzi wa mapema badala ya kupita kwenye magari kama wanakwenda kuwinda wanyama.
Wakati huo huo Kamanda Msangi amedai kuwa katika kipindi hiki pia jeshi hilo limeanzisha utaratibu mpya kwa kutawanya askari polisi katika maeneo mbalimbali hasa kwenye kata na tarafa ili kuwa karibu zaidi na wananchi ambapo mpango huo umeonyesha kuzaa matunda.
Pamoja na kutoa wito huo kwa askari polisi pia amedai kuwa vitendo vya kihalifu katika mkoa wa mbeya vimepungua kwa asilimia 18 kwa kipindi cha mwezi january hadi februali mwa huu.
TATHIMINI YA HALI YA UHALIFU MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA FEB-
2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JAN-
2014.
1. TATHMINI YA MAKOSA YOTE YA JINAI.
Katika kipindi
hicho cha Feb –2014 jumla ya makosa 2,003 yaliripotiwa, wakati kipindi kama
hicho mwezi Jan – 2014 makosa 2,438 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 435 sawa na asilimia 18.
2. TATHMINI YA MAKOSA MAKUBWA YA JINAI.
Katika kipindi
hicho cha Feb – 2014 jumla ya makosa
makubwa 196 yaliripotiwa, wakati
kipindi cha mwezi Jan-2014 makosa 212 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 16 sawa na asilimia 8.
3. TATHMINI YA MAKOSA YATOKANAYO YA JITIHADA
ZA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA WADAU WENGINE.
Aidha
katika kipindi cha Feb – 2014 makosa makubwa yatokanayo na jitihada za Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali
katika kufanya doria,misako na operesheni katika kupambana na uhalifu na
wahalifu yaliripotiwa matukio 40, wakati
kipindi mwezi Jan- 2014 yaliripotiwa
makosa 56, hivyo kuna pungufu ya matukio 16, sawa na asilimia 29.
4. TATHMINI YA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.
§ Kwa
upande wa makosa ya usalama barabarani jumla ya makosa/matukio yote
yaliyoripotiwa katika kipindi cha Feb –
2014 yakiwemo makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na
usafirishaji ni 3,817 wakati kipindi
mwezi Jan- 2014 yaliripotiwa makosa 4,416 hivyo kuna pungufu ya makosa 599 sawa
na asilimia 14.
§ Matukio
ya ajali yaliyoripotiwa kwa kipindi cha Feb
– 2014 yalikuwa 29 wakati kipindi cha Jan-
2014 yalikuwa 38 hivyo kuna upungufu wa matukio 9 sawa na asilimia 24. Matukio ya ajali za vifo yaliyoripotiwa Feb – 2014 yalikuwa 15 wakati
kipindi cha Jan-2014 yaliripotiwa
matukio 27 hivyo kuna pungufu ya matukio 12 sawa na asilimia 44.
§ Watu
waliokufa kipindi cha Feb- 2014 walikuwa 18 wakati Jan -2014
walikuwa 30 hivyo kuna pungufu ya watu 12, sawa na asilimia 40.
Watu waliojeruhiwa kipindi cha Feb – 2014 walikuwa
watu 22 wakati Jan – 2014 walikuwa watu 49 hivyo
kuna pungufu ya watu 27 sawa na asilimia 55.
§ Katika
kipindi cha Feb - 2014 jumla
ya makosa 3,788 ya ukiukwaji wa
sheria za usalama barabarani na usafirishwaji yalitozwa faini sawa na tozo la Tshs 100,920,000/= ikilinganishwa na tozo la Tshs 131,340,000/= iliyokusanywa
katika kipindi Jan - 2014 kutokana
na makosa 4,378, hivyo kuna pungufu la kiasi cha tshs 30,420,000/= sawa na asilimia 23.
5.
MAJEDWALI KUONYESHA HALI YA UHALIFU.
MCHANGANUO WA MAKOSA
YOTE MAKUBWA YA JINAI NA USALAMA
BARABARANI KWA KIPINDI CHA FEB - 2014
IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JANUARI, 2014.
MAKOSA
|
FEB–
2014
|
JAN
– 2014
|
TOFAUTI +/-
|
ASILIMIA %
|
MAKOSA DHIDI YA BINADAMU
|
||||
MAUAJI
|
17
|
22
|
-5
|
-23
|
KUBAKA
|
36
|
44
|
-8
|
-18
|
KULAWITI
|
5
|
6
|
-1
|
-17
|
KUTUPA MTOTO
|
-
|
1
|
-1
|
-100
|
USAFIRISHAJI BINADAMU
|
3
|
-
|
+3
|
+300
|
JUMLA
|
61
|
73
|
-12
|
-16
|
MAKOSA DHIDI YA KUWANIA MALI
|
||||
UNYANG’ANYI WA K/SILAHA
|
1
|
2
|
-1
|
-50
|
UNYANG’ANYI WA K/NGUVU
|
13
|
9
|
+4
|
+44
|
UVUNJAJI
|
36
|
26
|
+10
|
+38
|
WIZI
|
291
|
440
|
-149
|
-34
|
WIZI WA PIKIPIKI
|
11
|
20
|
-9
|
-45
|
WIZI WA MIFUGO
|
18
|
15
|
+3
|
+20
|
JUMLA
|
370
|
512
|
-142
|
-28
|
MAKOSA DHIDI YA MAADILI YA JAMII
[YATOKANAYO NA JITIHADA ZA POLISI KWA USHIRIKIANO NA WADAU NA WANANCHI
MBALIMBALI]
|
||||
KUPATIKANA NA SILAHA
|
2
|
2
|
-
|
-
|
BHANGI
|
18
|
26
|
-8
|
-31
|
NYARA ZA SERIKALI
|
-
|
3
|
-3
|
-300
|
POMBE YA MOSHI.
|
17
|
15
|
+2
|
+13
|
WAHAMIAJI HARAMU
|
3
|
-
|
+3
|
+300
|
JUMLA
|
40
|
46
|
-6
|
-13
|
0.
MATUKIO YA USALAMA BARABARANI KWA KIPINDI
FEB - 2014 NA JAN 2014
|
||||
MATUKIO
|
3,817
|
4,416
|
-599
|
-14
|
MATUKIO YA AJALI
|
29
|
38
|
-9
|
-24
|
AJALI ZA VIFO
|
15
|
27
|
-12
|
-44
|
WALIOKUFA
|
18
|
30
|
-12
|
-40
|
WALIOJERUHIWA.
|
22
|
49
|
-27
|
-55
|
AJALI ZA MAJERUHI
|
14
|
11
|
+3
|
+27
|
MAKOSA YA UKIUKWAJI WA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA USAFIRISHAJI
|
3,788
|
4,378
|
-590
|
-14
|
TOZO [NOTIFICATION]
|
100,920,000/=
|
131,340,000/=
|
-30,420,000/=
|
-23
|
Post a Comment