Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Moja ya kazi za marehemu Steven Kanumba ambazo zimetajwa kuwa kuendelea kuwa bora katika soko la jijini mbeya

Mwenyekiti wa Chama Cha Wasanii jijini Mbeya Ndugu Samuel Mwamboma akizungumzia namna soko la filamu za kibongo zinavyopewa nafasi jijini humo ambapo amedai kuwa mpaka sasa bado filamu za marehemu Kanumba zimeendelea kupendwa zaidi  na wapenda filamu jijini humo .
 Amefafanua kuwa kupendwa kwa filamu za marehemu Kanumba kunatokana na ubora wa kazi zake ambazo zimeweza kuendana na soko la kiushindani la ndani na  nje ya Tanzania tofauti na filamu zinazochezwa na wasanii wengine wa hapa Nchini.

Amesema mafanaikio ya kanumba yanatokana na yeye mwenyewe kujitambua na kujua nini alichokuwa akikifanya kama msanii huku akiweka mazingira ya kuwainua wenzake tofauti wengine ambao wamajawa na ubinafsi na roho za kwanini.

Kutokana na hali hiyo Mwamboma amewataka wasanii wa jijini mbeya pamoja na wengine kwa ujumla kujituma kwa bidii pamoja na  kujitambua kuwa wananafasi gani katika kukuza kazi zao badala ya kujibweteka.

Amesema katika jiji la Mbeya kuna zaidi ya vikundi 48 vya wasanii lakini ndani ya wasanii hao bado wengi wao  hawajajitambua kuwa wao ni akina nani hivyo amewataka kuacha tabia hiyo na kujituma zaidi ili kufikia malengo badala ya kuendelea kulalamika kila kukicha kwa filamu haziwanufaishi.

Bwana Mwamboma akionyesha moja ya kazi za wasanii zinazofanya vizuri katika soko la filamu jijini humo.




PICHA NA JAMIIMOJA

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top