Baadhi ya Akina mama wakiserebuka katika viwa ja hivyo vya CCM Ilomba kufurahia siku yao. |
Mmoja wa wanaharakati wa kutetea haki za akina mama jijini Mbeya Mama Jenny Lawa akipaza sauti yake katika maadhimisho hayo. |
Akina Baba nao hawakuwa Nyuma katika kuwa sindikiza akina mama kusherekea siku yao |
Burudani nazo hazikuwa nyuma sana katika kusindikiza siku ya wanawake duniani |
Na EmanuelMadafa,mbeya
Wito umetolewa kwa wanawake jijini mbeya kuhakikisha wanaacha tabia ya kulalamika na kukata tamaa badala yake wajikite katika kufanya kazi kwa bidii na kutumia fursa walizo nazo.
Kauli hiyo imetoleaa leo jijini Mbeya na Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Mbeya Dr Marry Mwanjelwa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani ambapo kila mwaka husherekewa machi8 ambapo pia kilele cha maadhimisho hayo kwa jiji la mbeya zimefanyika katika viwanja vya ccm Ilomba.
Akizungumza katika maadhimisho hayo mbunge huyo amedai kuwa umefika wakati wanawake wakaacha tabia ya kulalamika badala yake watumie fursa walizo nazo katika kujiingizia kipato.
Amesema umefika wakti sasa wanawake wote wakajitambua na kuacha tabia hiyo kwani imechangia kwa kiwango kikubwa kuendelea kuleta manyanyaso kwa mwanamke huyo.
Hata hivyo Mbunge huyo amesisitiza suala la kujiamini kwa akina mama ili kuleta chachu ya mabadiliko dani ya familia na jamii kwa ujumla badala ya kuendelea kutegemea mwanaume kwa kila jambo katika suala la maamuzi.
Pamoja na kuwataka akina mama hao kutambua fursa na kujiamini pia amessistiza suala la kupendana wao kwao ili kuleta nguvu ya pamoja katika kupigania haki zao.
Kwa upande wao baadhi ya akina mama waliohudhuria sherehe hizo wametoa wito kwa mashirika mbalimbali ya kijamii kuendelea kutoa elimu kwa akina mama wengine walipo maeneo ya vijini ili kusaidia kuleta mabadailiko zaidi .
mwisho.
Post a Comment