Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani A. Mungi akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa na kuwambia namna Jeshi hilo lilivyojipanga kulinda amani na kuwasihi wananchi wote wa Kalenga kujitokeza na kwenda kupiga kura kwa amani.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Iringa Ramadhani A. Mungi akizungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza namna walivyojipanga kulinda amani siku ya uchaguzi Kalenga na kuhakikishia wananchi wa Kalenga kuwa jeshi la Polisi limejipanga kupambana na wahalifu ,leo tarehe 14 Machi 2014.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI
JESHI
LA POLISI TANZANIA
“PRESS
RELEASE”
Ndugu waandishi
wa habari , kwa niaba ya askari Polisi wa Mkoa wa Iringa, nitumie fursa hii
kuwakaribisha hapa ofisini kwetu.
Ndugu zangu
tumeitana hapa asubuhi hii ili niweze kuwapa taarifa ya usalama katika Mkoa
wetu wa Iringa hususani katika Jimbo la Kalenga katika kipindi hiki cha kampeni
za uchaguzi wa Jimbo la Kalenga na usalama wa siku ya uchaguzi wenyewe.Ili iwe
rahisi kueleweka taarifa hii nitaitoa kwa kifupi sana kwa kuigawa katika maeneo
matatu. Eneo la kwanza ni juu ya wapi tunataka tupafikie ( Where
we want to go ), eneo la pili ni lile la wapi tulipo ( Where are we? ) na eneo la tatu ni jinsi gani tutafika huko ( How do we get there ). Tuanze na
wapi tunataka tupafikie. Sisi Polisi
Mkoa wa Iringa
tunataka wananchi wa Kalenga wapinge
kura kwa amani
na utulivu mkubwa
siku ya jumapili
tarehe 16/3/2014. Hii ndio dila
yetu na tutahakikisha
tunafika hapo.
Kuhusu wapi
tulipo sasa, naomba niwaelezeni
kwa ufupi sana
matukio ya kijinai
kuanzia tarehe 19/02/14 mpaka
leo. Ndugu zangu, kuanzia tarehe
hiyo mpaka tarehe
2/03/2014 takribani
wiki mbili hakukuwa
na tukio lolote la uvunjifu wa
amani lililokuwa limepokelewa
katika vituo vyetu
vya Polisi. Hali
ilianza kubadilika tarehe
3/3/2014 ambapo
baadhi ya waandishi
walifika ofisi kwangu
na kunieleza kuwa
kumetoka kwenye mkutano
wa CHADEMA ambapo
wameelezwa na chama
hicho kuwa usiku
wa siku hiyo
walimkamata mtu mmoja
kwa kosa la
kujaribu kuchoma moto
nyumba waliokuwa wakiishi
wafuasi wao katika
kijiji cha WASA. Waandishi hao
walinitaka nithibitishe kutendeka
kwa kosa hilo
na walieleza kuwa
wameelezwa kuwa bado
halijaripotiwa kituoni. Mimi nilikataa
kusema lolote kuhusu
hilo kwani lilikuwa
bado halijaripotiwa Polisi.
Tarehe 4/03/2014 nilifuatwa tena
na baadhi ya
waandishi na kunieleza kuwa
siku hiyo waliitwa
na CCM na
kuelezwa kuwa siku
ya tarehe 27/2/2014 walitegewa
misumari katika kijiji
cha WASA ili
mabasi yaliyokuwa yamebeba
wafuasi wao yaweze
kutobolewa magurudumu yake, pia
nao walisema tukio
hilo halijaripotiwa Polisi. Mimi
nilikataa kulizungumzia swala
hilo.
Ndugu wanahabari, vitendo
vilivyofanywa na vyama
hivyo vililenga kuanzisha
propaganda za kisiasa
kwa kutumia uhalifu
kwa kupitia vyombo
vya habari. Sisi Polisi
tulibaini hali hiyo
na ndiyo sababu
tuliamua kuwa kimya
na nyinyi wenzetu
kwa kuzingatia maadili
ya kazi zenu
pia mlikaa kimya.
Kuanzia hapo vyama
vilianzisha mashindano ya
kuripoti kesi zao
Polisi. Leo hii vyama
hivyo vimeripoti kesi
ishirini na moja
ambazo zilisababisha kukamatwa
kwa wafuasi (19) wa vyama hivyo viwili.
Ndugu waandishi,
kati ya kesi hizo ishirini na moja, kesi kumi na tisa (19) zile ambazo hazina
madhara ya moja kwa moja kwa binadamu ama mali, kesi hizo ni zile ndogondogo sana, kama vile kuchana
mabango, kuteremsha bendera, kuchana vipeperushi, kutukanana n.k. kesi tatu
zilikuwa zile zenye madhara kwa binadamu na mali ambazo ni kupigana hadharani,
kujeruhi na kuharibu mali. Kati ya kesi ishirini na moja (21), kesi kumi
upelelezi wake umekamilika na majalada yake yamefikishwa kwa mwanasheria wa
serikali.
Ndugu waandishi,
katika kesi hizo Polisi tumeibaini mengi mfano CHADEMA kilikuwa kikitoa
malamiko kuwa tumeacha kumkamata ndugu hassan mtenga mtuhumiwa wa kesi moja
iliyokuwa imefunguliwa dhidi yake. Shutuma hizo hazina msingi kwani kesi
iliyofunguliwa dhidi ya mtu huyo haikuwa ya jinai bali ya madai na
tuliwajulisha hivyo. Nia ya kufanya hivyo ilikuwa kuifanya jamii iamini kuwa Polisi
ni dhaifu na wenye kuonyesha upendeleo katika kushughulikia kesi za uchaguzi.
Nashukuru Polisi tulikuwa watulivu, hatukujibu na jamii imetuelewa sana.
Ndugu waandishi,
sijui mlijulishwa na nani kwamba Padri mmoja alifungwa kamba na alipingwa na
kuburuzwa. Nanyi bila ya kuthibitisha kwetu mkaandika habari hiyo. Tuwaeleze
kuwa mtu huyo ni miongoni mwa watuhumiwa tuliowakamata katika moja ya makosa
yaliyotendeka, tulimhoji, aliandikwa maelezo yake na alipewa dhamana. Hata siku
moja hajawahi kutoa taarifa Polisi juu ya matukio aliyotendewa. Nia ya
kutangaza taarifa hiyo ni kuzua hofu kwa wananchi na kutaka kuchochea chuki kwa
wafuasi wa dhehebu lake na wale wa dini yake.
Ndugu waandishi,
pamoja na matukio hayo polisi tumekuwa tukipokea taarifa za vitisho vya kuwepo
kwa watu mbalimbali kutoka kwa vyama vyote walioingizwa mkoani humu kwa nia ya
kutenda vitendo vya uvunjifu wa amani. Aidha, tumewasikia viongozi wa vyama
wakitamba kuingiza maelfu ya watu mkoani mwetu. Kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo
Arusha, Mbeya kwa visingizio vya kulinda kura.
Sasa nataka
niwaeleze kuwa sheria iko wazi kabisa, kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na
wakala wa chama kinachoshiriki katika uchaguzi huo na hao ndio wawakilishi wa
chama hicho na walinzi halali wa uchaguzi ni askari wa Jeshi la Polisi.
Kufuatia hali hiyo mambo yafuatayo yanasisistizwa sana.
1. Hatutaki
kuona walinzi wa chama chochote katika Jimbo la Kalenga. Jukumu la kulinda
uchaguzi, maisha na mali ya wana Kalenga ni la JESHI LA POLISI.
2. Hatutaki
kuona watu wasiokuwa na shughuli maalumu wanapitapita katika maeneo ya kupigia
kura.
3. Siku
ya uchaguzi si siku ya kampeni. Hatutaki kuona helikopita za vyama
vyote zenye kuashiria kufanya
kampeni.
Nawaasa
watu wote hasa wale waliotoka nje ya Iringa, sisi huku Iringa tunapenda sana
amani kuliko kitu chochote kile hivyo ikiwa wameletwa kama MAJESHI YA KUKODIWA ili kuharibu amani ya Kalenga kama walivyozoea
kufanya huko walikotoka, Sisi Polisi na wana Kalenga tupo imara, tumejipanga
vizuri kukabiliana nao.
Aidha,
napenda kuwatoa hofu wana kalenga, wasiwe na wasiwasi kabisa, sisi Polisi Iringa
tupo imara na tumejipanga vizuri katika kuwalinda kikamilifu. Nawaomba
wajitokeze kwa wingi sana siku ya kupiga kura na wapige kura zao kwa uhuru
kabisa.
Ndugu
waandishi, nawashukuru sana kwa jinsi mlivyofanya kazi zenu kwa ueledi mkubwa.
Hata siku moja hatujawahi kusikia ama kusoma habari za uchochezi kwa kushabikia
chama chochote kile.
AHSANTENI SANA.
Post a Comment