Wito umetolewa kwa serikali
mkoani Mbeya kuhakikisha inaanza mikakati ya kutoa elimu kwa wakulima na
wananchi mkoani humo juu ya kuachana na kilimo cha mazoea.
Kauli hiyo imetolewa na Mmoja
wa wakulima wa zao la Kokoa Mkazi wa Mabunga Kata ya Ipinda Wilayani Kyela
Mkoani Mbeya Ndugu Masdeni Mwaipungu ambaye amedai kuwa kwa asilima kubwa
wakulima wa ukanda huo bado wamejikita katika kilimo cha kizamani cha mazoea.
Amesema endapo serikali
itaanzisha mikakati ya kutoa elimu kwa wakulima juu ya kuachana kilimo cha
mazoea na kuanzisha kilimo cha kisasa anaamini mkulima huyo atapata manufaa makubwa
na kufikia malengo yake.
Mkulima huyo amedai kuwa yeye
kwa upande wake aliamua kujikita katika shughuli za kilimo toka mwaka 1967 ambapo
kwa mara ya kwanza aliamua kupanda mazao ya kudumu kwa kufuata njia za kitaalam
hali ambayo imemfanya aendelee kunufaika na kilimo chake.
Amedai kuwa katika kipindi
hicho kulikuwa na ardhi ya kutosha yenye rutuba hivyo kama angejikita katika zoa moja pekee bila
kupanda zao la kudumu asinge weza kufikia malengo yake ambapo kwa zao hilo kilomoja ni shilingi elfu 2500.
Amesema kwa kipindi cha
miezi minne ana uhakika wa kuingiza fedha na kukikidhi
mahitaji yake tofauti na mkulima wa
kawaida anaye lima mahindi na mazao mengine.
Kutokana na hali hiyo mzee huyo
ameitaka serikali
kutambua kuwa lengo la
mkulima haliwezi kufikiwa kama hakutakuwa na nguvu ya kutosha kwa kuhakikisha mkulima huyo anapatiwa elimu juu
ya kufuata njia bora za kilimo.
kwa viongozi hao
Post a Comment