Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwenyekiti wa Mtaa wa Inyala Kata ya Iyunga Jijini Mbeya Ndugu Nelson Mahena akielekeza eneo lenye ubovu ambalo ndio kero kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.



moja ya eneo la barabara itokayo Mbembela Kata ya Nzovwe jijini mbeya Kuelekea Inyala Kata ya Nzovwe jijini humo ambayo ndiyo barabara muhimu kwa wakazi wa pande zote mbili .
 

Daraja la Mto Nzovwe ambalo ndio kiunganishi kati ya wananchi wa Mtaa wa Inyala Kata ya Iyunga  jijini mbeya na wananchi wa Mbembbela Kata ya Nzovwe ambalo limekuwa mkombozi kwao .

Moja ya kipande cha Barabara  ambacho kimekuwa kero kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo hasa katika kipindi cha Mvua ambapo magari hushindwa kupita na kusababisha usumbufu mkubwa mara msaada wa haraka unapo hitajika kwa kupeleka wagonjwa katika kituo cha Afya cha Ikuti na kulazimika kutembea kwa miguu  kwa kupandisha kilima hicho.

Mmoja wa Wananchi wa eneo hilo ambaye amezungumzia hali hiyo na kudai kuwa kuwepo kwa ubovu wa barabara hiyo kumechangia kwa asilimia kubwa baadhi ya wananchi wa eneo hilo kutapeliwa na watu wanao dai kuwa wamekuja kurekebisha barabara hiyo kwa kuwatoza kiasi cha shilingi elfu 50 kama sehemu ya kukamilisha vipimo kwa kujitambulisha kuwa wao ni watumishi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya.

Picha na Jamii Moja.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top