Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Watu 37
wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya kwa kosa la kufanya fujo na
kuharibu mali.
Akizungumzia Tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Ahmed Msangi amesema kuwa tukio hilo limetokea Aprily 11 mwaka huu majira ya
saa 10:30 asubuhi huko katika
eneo la iyela - airport, kata ya iyela,
jijini Mbeya ambapo kundi la watu wakiwemo waendesha
pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zaidi ya
mia mbili walivamia kwenye msiba wa marehemu siza john mwambenja [28] mwendesha pikipiki @ bodaboda, mkazi wa airport na kufanya fujo ikiwa ni pamoja na kuharibu
mali mbalimbali katika nyumba hiyo.
Amesema Lengo la Bodaboda hao ilikuwa kushinikiza
kumkamata mtalaka wa marehemu Ndugu Oliva
herode mwamlima [ 25] mkazi wa forest mpya ambaye alikuwepo katika msiba
huo kwa madai kuwa anahusika na njama za mauaji ya aliyekuwa mume wake kutokana na kuachwa kwa
sababu za matatizo ya kifamilia.
Amesema kuwa Marehemu Siza Johnjohn aliuawa na
mtu/watu wasiofahamika na mwili wake kukutwa umetupwa kando ya reli ya
tazara tarehe 09.04.2014 ukiwa na jeraha
la kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kando yake kutelekezwa
pikipiki yake mpya yenye namba za
usajili t. 932 ctz aina ya kinglion.
Kamanda Msangi amebainisha kuwa Kufuatia vurugu hizo
zilizozimwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya, watu 37 walikamatwa na kufikishwa
mahakama ya mwanzo mbeya mjini ambao walisomewa mashitaka yao shauri la jinai
namba 291/2014.
Watuhumiwa wote wamepelekwa mahabusu gereza la ruanda
ambapo kesi itaanza kusikilizwa 14.04.2014.
Aidha katika vurugu hizo mali za jeshi la polisi gari
moja la kituo cha polisi kati 474 aina
ya land rover 110 liliharibiwa kwa kupigwa mawe na kuvunjwa
kioo kikubwa cha mbele. Hakuna madhara ya kibinadamu yaliyoripotiwa kutokea
wakati wa vurugu hizo na hali ya amani ilirejea kuwa ya kawaida na wananchi
wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi
mwandamizi wa polisi ahmed z. Msangi anatoa
wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake
wahakikishe wanawafikisha katika mamlaka husika watuhumiwa wanowakamata kwa
tuhuma mbalimbali ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.
Aidha anatoa rai kwa jamii kujenga tabia ya kuheshimu mamlaka zilizowekwa kisheria ikiwa
ni pamoja na vyombo vya dola ili kuepuka matatizo yanayoweza kuepukika badala
ya kuleta ushindani na vurugu. Pia kamanda msangi amesisitiza kuwa jeshi la
polisi halitasita kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote
wanaokaidi na kuleta vurugu.
Mwisho.
picha na Jamiimojablog.
Post a Comment