Na EmananuelMadafa,Mbeya
KIKOSI cha vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam FC, Teyari kimewasili jijini mbeya kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu sokaTanzania Bara dhidi ya wenyeji Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini humo.
Azam
fc wanaohitaji pointi tatu ambazo zitawapa ubingwa rasmi na kuwavua
mabingwa watetezi, Dar Young Africans.
Kocha
Mcameroon wa Azam FC, Joseph Marius Omog alikuwa mwenye furaha baada ya ushindi
wa 3-0 juzi Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani dhidi ya wenyeji Ruvu
Shooting, lakini akasema shughuli haijaisha.
“Ni
furaha. Ni ushindi mzuri, tumevuka kikwazo kimoja, vijana waliuanza mchezo
vizuri wakizingatia nilichowaambia. Karibu kila mmoja alitekeleza majukumu yake
vizuri. Wapinzani walikuwa wagumu, lakini tumechukua pointi tatu,”alisema.
Omog
alisema anajivunia wachezaji wake na hana cha kuwaambia zaidi ya asante pamoja
kama timu na akawataka kuendeleza mshikamano huo daima.
Hata
hivyo, Omog amewaambia wachezaji wake kwamba wanahitaji kushinda pia mechi
mbili za mwisho ili wamalize ligi vizuri.
Ushindi
huo umeifanya Azam FC ifikishe pointi 56 baada ya kucheza mechi 24 na kujivuta
karibu kabisa na chumba kinachohifadhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu, ikiwaacha
kwa pointi nne mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 52 za mechi 24 pia.
Timu
hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake, baada ya mechi
ya kesho itacheza mechi ya mwisho dhidi ya JKT Ruvu Aprili 19, Uwanja wake wa
Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
CHANZO:
TOVUTI YA AZAM
Post a Comment