Na Jamiimojablog
Hifadhi ya Kitulo awali ilijulikana kama Elton Plateau baada ya Mvumbuzi Fredrick Elton kupita eneo hilo mnamo mwaka 1870. Mwaka 1960 Shirika la Chakula na Kilimo(FAO) ilichukua eneo hili kwa ajili ya ukulima wa ngano na ufugaji wa kondoo.
Baadaye ikageuzwa kuwa shamba la ng'ombe ambalo lipo hadi leo hivyo basi . Kutokana na umuhimu wa eneo hilo wadau mbalimbali wa mazingira walipendekeza eneo hilo litangazwe kuwa hifadhi ya taifa ili kulinda umaridadi wa maua na mimea adimu inayopatikana ndani ya eneo hili.
Mwaka 2005, Kitulo ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa ikijumuisha sehemu ya eneo la shamba la mifugo, Msitu wa Livingstone na bonde la Numbi kiasi cha kilometa za mraba 412.9 ndani ya mwinuko wa mita 2100 na 3000.
Hifadhi hii inasifika kwa kuwa na maua aina mbalimbali na zaidi ya aina 30 hupatikana Kitulo pekee na maeneo kusini mwa Tanzania.
Maua ya
Kitulo ndilo eneo pekee Tanzania ambapo ndege aina ya Tandawili machaka (Denhams
Bustard) wana makazi. Wapo aina mbalimbali ya ndege kama vile Mpasua mbegu mweusi (Kipengere
seed eater) na wengineo.
Jamii mpya ya nyani (Lophocebus Kipunji) waligunduliwa mwaka 2003 Kitulo. Hifadhi hii ina uwanda wa tambarare, mabonde, vilima na maporomoko ya maji. Ndani ya msitu, kuna miti aina ya cidar yenye urefu wa zaidi ya mita 50 na inakadiriwa kuwa mirefu kuliko yote duniani.
Kitulo inafikika kwa gari kutoka Chimala, kilometa 78 Mashariki mwa mji wa Mbeya. Reli ya TAZARA hupita karibu na hifadhi ya kitulo. Pia unaweza kufika ukitokea Zambia kupitia Tunduma au Malawi kupitia Karonga kwa barabara.
Post a Comment