Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi |
Na EmanuelMadafa,MBEYA
Mfanyabiashara mmoja Mkazi wa Kyela Mkoani Mbeya Jail Mrbange( 57)amekutwa amejiua kwa kujichoma kisu shingoni katika chumba alichopanga jijini
mbeya.
Tukio hilo limetokea jijini Mbeya katika nyumba
ya kulala wageni iitwayo ten commandment
iliyopo eneo la stendi kuu April 11 mwaka huu majira ya saa 10:30
asubuhi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema Chanzo
cha tukio hili bado kinachunguzwa, ingawa
uchunguzi wa awali unaonyesha marehemu
alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya
kisukari na bp kwa muda mrefu.
Amesema Marehemu alichukua chumba April 10
mwaka huu majira ya saa 11:00 jioni na alifanya kitendo hicho baada ya kujifungia kwa ndani katika chumba namba 13 kisha
kujiua na kisu.
Amesema Kisu alichokitumia kijiua kilikutwa bado kipo
shingoni. Aidha marehemu hakuacha ujumbe
wowote ambapo Mwili wake ulikutwa ndani katika baada ya askari polisi kwa
kushirikiana na wenye nyumba kuvunja mlango.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi
mwandamizi wa polisi ahmed z. Msangi anatoa
wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ina madhara
kwa jamii.
Mwisho.
Post a Comment