Kocha Msaidizi Timu ya Taifa ya Maboresho Ndugu Salum Mayanga akitanga Majina ya wachezaji 16 walioteuliwa kujiunga na Timu ya Taifa Leo Jijini Mbeya. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
JOPO la Makocha wa Timu ya Maboresho
waliweka kambi Mjini Tukuyu Rungwe Mbeya limetangaza majina ya wachezaji 16
waliopataikana katika mchakato wa maboresho ya timu mpya ya taifa ya Tanzania.
Vijana hao 16 ni kati ya 33
waliopatika katika mchakato wa kutafuta vijana wenye vipaji kwa lengo la kupata
timu mpya ya Taifa mchakato ambao ulihusisha mikoa yote ya Bara na Visiwani ambapo kambi hiyo ilianza kuanzia Machi 22 mwaka huu .
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Hapa Kocha Msaidizi wa Kikosi hicho
ca Maboresho Ndugu Salum Mayanga amesema teyari hatua ya awali ya kuwapata
vijana 16 imekwisha fanyika wakati wakiwa kambini hapo Mjini Tukuyu Mbeya.
Amewataja wachezaji waliochaguliwa
katika mchakato huo kwa upande wa walinda mlango kuwa ni Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara).
Kwa upande wa mabeki wa pembeni
waliochaguliwa katika mchakato huo ambao upo chini ya udhamini wa Kilimanjaro
Premium Lager ni Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Omari Kindamba (Temeke) na Shiraz Abdallah
(Ilala).
Mabeki wa kati ni Yussuf Suleiman
Mlipili (Temeke)Abbas na Said Juma Ali
(Mjini Magharibi)huku Viungo wakiwa ni
Abubakar Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magoma (Shinyanga).
Abubakar Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magoma (Shinyanga).
Huku viungo wa pembeni ni Ommar
Athuman Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara)
Washambuliaji ni Abrahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael
Bundara ,(Ilala) Ayubu Hashim Lipati (Ilala), Mohamed Seif Said (Kusini Pemba),
Hata hivyo amesema wachezaji wengine
waliungana na wale 16 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga)na Bayage Atanas Fabian (Mbeya)kutoka
timu ya vijana wenye umri (160)
Amesema Wachezaji hao 16 wataungana
na wale wa Taifa Stars watakaoingia kambini Aprili 22 mwaka huu.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mapema mwezi Mei mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.

Pamoja na kutaja kikosi hicho pia
amesema kuwa katika wale vijana walienguliwa katika kikosi hicho Tayari TFF
imewaka utaratibu mzuri namna ya kuwatumia kwa hapo baadaye na pale watakapo
hitajika.
Timu
hiyo itakuwa chini ya Madadi akisaidiwa na makocha Hafidh Badru, Salum Mayanga
na Patrick Mwangata. Aprili 13 mwaka huu utafanyika mchujo ili kupata wachezaji
wa mwisho watakaoungana na wale wa Taifa Stars watakaoingia kambini Aprili 22
mwaka huu.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mapema mwezi Mei mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mapema mwezi Mei mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
MWISHO
Vijajna wakiendelea na Mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Msasani Tukuyu Mbeya Picha na Jamiimojablog. |
Post a Comment