Profesa Kihanga akizungumza na baadhi ya watoto hao kabla ya kukabidhiwa ka msaada kwa mama malezi wa kituo hicho. |
Baadhi ya wanajumuiya hao wakikabidhi msaada kwa mama mlezi wa kituo hicho Bi.Anna Kasile. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Jumuiya ya Chuo Kikuu Mzumbe Cumpus ya Mbeya imeungana watoto yatima Mkoani
Mbeya na Baadhi ya maeneo Mengine Nchini Katika Kusherekea Kilele cha Sherehe za Muungano.
Jumuiya hiyo ambayo ni mchanganyiko wa wanafunzi walimu na watumishi wote wa chuo hicho
wameungana kwa pamoja na kutoa msaada wa chakula pamoja na mahitaji mengine
katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Malezi ya Huruma kilichopo Simike
jijini Mbeya msaada wenye thamani ya zaidi ya shilingi mil2.
Akikabidhi Msaada huo kwa niaba ya wanajumuiya hao
Mkuu wa chuo cha Mzumbe Campus ya Mbeya Prof.Kihanga Ernest amesema hatua ya
kutimiza miaka 50 ya muunghano wa Tanzania ni furaha kubwa hivyo wao wameamua kufurahi na watoto wanaoishi
katika mazingira magumu.
Amesema isingekuwa vyema kusherekea sherehe hizo
wakati kunawatu wanaishi katika mazingira magumu na wanahitaji msaada kwa
mahitaji mbalimbali hivyo msaada huo
nisehemu ya kuifanya jamii kama hiyo ifurahi kwa pamoja katika sherehe hizo.
Hata hivyo profesa huyo amesema muungano huo
umekuwa na amani kubwa sana hivyo hata vijana hao wanahitaji kufahi na kuiona
faida hiyo ili nao waweze kujua historia na hatimaye kuendelea kuulinda
muungano huo.
Amefafanua kuwa pamoja na muungano huo kudumu kwa miaka 50 lakini pia
umetoa fursa kwa vijana walio wengi kupata elimu bila kujali Uzanzibari
na Utanganyika pamoja na kuitangaza vyema Tanzania Kimataifa kama sehemu ya
Amani .
Kufuatia hali hiyo Profesa Kihanga amelitaka bunge Maalum la katiba
kuhakikisha wanangalia kwa umakini mkubwa suala la kuulinda
muungano huo .
Aidha Kwa upande wake Mratibu wa shughuli hizo ambaye
pia ni Mhadhili wa chuo hicho Ndugu Steven John amesema kuwa tofauti na kusherekea
miaka 50 ya Muungano lakini pia wameona washirikiane na
jamii ili isionekane kuwa chuo kikuu ni sehemu ya kusoma tu badala yake iwe
sehemu ya jamii.
Amesema
wameamua kuonyesha mjumuiko wao na watu wanaowahitaji msaada ili kuweza kuleta nuru ya siku ya muungano
kwani wanamini kuwa yapo mengi wanayohitaji lakini kwa kufanya hivyo kutaleta
faraja kubwa kwa kundi hilo.
Amesema msaada uliotolewa na wanajumuiya hao ni
michango toka katika mifuko yao binafsi bila kuhusisha taasisi hiyo ya Mzumbe .
Akipokea msaada huo Mama mlezi wa kituo hicho Ndugu
Anna kasile amesema msaada uliotolewa na wanajumuiya hao umefika katika siku
muafaka hasa kutokana na kuwepo kwa uhaba wa chakula katika kituo moja wapo kati ya hivyo kilichopo
Morogoro ambacho nacho kipo chini yake.
Amesema msaada huo utagawanywa ambapo chakula kingine
kitasafirishwa na kupelekwa mkoani
humo hivyo amewashukuru wanajumuiya hao kwa kuonyesha upendo kwa watoto hao.
Amesema katika kituo hicho cha Simike kinajumla ya
watoto 150 ambao wanahitaji gharama kubwa katika kuwahudumia hivyo msaada huo
utawasaidia kwa kiasi kikubwa.
mwisho
Post a Comment