Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

 

1Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama katikati akiwa katika picha ya pamoja na baba yake mzazi Mzee Mwita na mmoja wa waratibu wa tamasha la pasaka Bw. wakati walipofika katika hospitali ya muhimbili ili kumjulia hali kutokana na majeraha na maumivu ya ajali aliyoipata wiki iliyopita wakati akielekea mkoani Dodoma kwa shughuli zake, watu wengi wamemtembelea hospitalini hapo leo akiwemo Askafu Bruno Mwakibolwa wakanisa la EAGT ,Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba na watoto wa kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa kutoka Mbweni jijini Dar es salaam.(FULLSHANGWE NA KIKOSIKAZI CHAKE TUNAKUTAKIA AFYA NJEMA MUNGU AKUPONYE HARAKA UREJEE KATIKA KAZI YA KUMTUMIKIA MUNGU) 2Alex Msama akifungua mlango wa chumba chake alimolazwa ili kusalimiana na baadhi ya wageni waliomtembelea hospitalini hapo. 3Alex Msama akitoka nje ya chumba chake alimolazwa ili kusalimiana na baadhi ya wageni waliomtembelea hospitalini hapo. 4Alex Msama akifelezea jambo kwa baadhi ya wageni waliomtembelea hospitalini hapo. 6Askafu Bruno Mwakibolwa wakanisa la EAGT akimsalimia Alex Msama wakati aliomtembelea hospitalini hapo kumjulia hali. 7Askafu Bruno Mwakibolwa wakanisa la EAGT akisoma neno takatifu la kumtia faraja Bw. Alex Msama ili aendelee na kazi ya mungu wakati aliomtembelea hospitalini hapo. 8 Watoto yatima cha Mwandaliwa kutoka Mbweni jijini Dar es salaam wakimjulia hali Bw. Alex Msama wakati walipomtembelea katika hospitali ya Muhimbili na kumjulia hali leo 9Watoto yatima cha Mwandaliwa kutoka Mbweni jijini Dar es salaam wakimuombea dua Bw. Alex Msama wakati walipomtembelea katika hospitali ya Muhimbili na kumjulia hali leo 10Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akimjulia hali Bw. Alex Msama wakati alipomtembelea katika hospitali ya Muhimbili leo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top