![]() |
Mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho jana lihifadhiwa akisimulia namna alivyokuwa akifanyiwa ukatili huo |
![]() |
Shangazi wa mtoto huyo Upendo Ngongi akisimulia kwa machungu namna mtoto wa kaka yake alivyofanyiwa ukatili huo. |
![]() |
Kamanda wa Polisi mbeya Ahmed Msangi |
Na
EmanuelMadafa,Mbeya
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida Mtoto wa kiume wa darasa la kwanza mwenye umri
wa miaka saba, amekuwa akifanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa
kuingiliwa kinyume cha maumbile(kurawitiwa) ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.
Mtoto huyo
ambaye jina lake limehifadhiwa, inadaiwa alianza kufanyiwa vitendo hivyo na
mwanachuo Daudi Anania umri
unaokadiliwa kuwa 27 kutoka chuo cha Ufundi cha Veta kilichopo ndani ya Jiji la
Mbeya, tangu akiwa na umri wa miaka sita kipindi hicho akiwa anasoma elimu ya
awali.
Blog hii lilifanikiwa kuzungumza na mtoto huyo, ambaye
hivi sasa ameanza matibabu baada ya vipimo kutoka kwa daktari wa
hospitali ya Rufaa ya Mbeya kuonyesha ya kwamba mtoto huyo amethirika zaidi
kwenye njia ya mkojo ambako kumekutwa na uvimbe na sehemu ya haja kubwa ikiwa
tayari imeharibiwa.
Akisimulia
mkasa huo, mtoto huyo amesema kuwa mwaka 2013 akiwa anaenda shule (elimu ya
awali) njiani alikutana na kijana huyo ambaye alimueleza ya kwamba waende
wote nyumbani huku akimuhahidi kumnunulia biskuti na juice.
Amesema,
wakiwa nyumbani kijana huyo alimpandisha kitandani na kumvua nguo kisha kumpaka
mafuta kwenye sehemu ya haja kubwa na kisha kumuingili huku akimtaka asipige
kelele na endepa atakahidi agizo hilo basi atammaliza kwa kisu ambacho
inasemekana alikuwa amekiweka pembeni.
“Tulipofika
nyumbani tuliingia chumbani ,alinipandisha kitandani na kunivua nguo
kisha kuniingilia huku akinitishia nisipige kelele kwani atanimaliza kwa
kunichinja kwa kisu na alipomaliza alinifuta na kunipaka mafuta kisha
kunirudisha nyumbani tena akinisisistizia ya kwamba nisiseme kwa mtu,”alisema
mtoto huyo.
Aidha,
kijana huyo aliendelea na mchezo huo mpaka siku ilipobainika baada ya majirani
kuingiwa shaka na tabia ya mtoto huyo ambaye ilianza kubadilika kwa kuchelewa
kurudi nyumbani na mara alipowasili alikuwa akitembea kwa tabu tena macho
yake yakiwa yameiva kwa kulia.
“Mara ya
kwanza ya kubaini mtoto huyu amefanyiwa unyama huu ni Juni, 2013 tarehe
sikumbuki siku hiyo alirudi nyumbani akiwa anatembea kwa tabu sana ndipo
nilipomuita mama yake na kumweleza wasiwasi wangu ambapo tulimkalisha chini na
alipobanwa alikiri kufanyiwa kitendo hicho na ndipo tulipomueleza shangazi
yake,”alisema jirani ambaye hakuta jina lake liandikwe.
Shangazi
wa mtoto huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Upendo Ngongi (31) mkazi wa
eneo la Itiji Jijini Mbeya,aliambia blog hii kwamba mara tubaada ya kupata taarifa hiyo alifika kwenye eneo la
tukio na kushuhudia mtoto huyo akiwa ameharibiwa.
“Nilipomkagua
mtoto nilishuhudia unyama huo ulivyofanyika hivyo nilichukua jukumu la
kumweleza baba wa mtoto ambaye ni kaka yangu ambaye alitutaka twende kituo cha
polisi kutoa taarifa kisha tumpeleke mtoto hospitali,’’alisema.
Amesema,
wakiwa njiani kuelekea kituo cha polisi alipigiwa simu na kaka yake ambaye
ndiye baba wa mtoto na kumtaka warudi nyumbani na waachane na masuala ya
polisi.
“Nilishtuka
sana mara baada ya kusikia kauli ya kaka ikiniambia nirudi nyumbani niachane na
masuala ya polisi, nilitii agizo lake na kurudi nyumbani lakini nilipomuhoji
kwanini amechukua maamuzi haya aliniambia ya kwamba yeye hataki ugomvi na
majirani,”alisema.
Amesema,
kitendo cha kwenda polisi kitamletea yeye matatizo ya kugombana na majirani
wakati wao si wenyeji wa Mbeya hivyo ni vema amuondoe mtoto kwa kumrudisha
nyumbani Songea.
“kweli
kaka alimrudisha mtoto nyumbani lakini mwezi wa kwanza (January
2014)alimrudisha Mbeya kwa ajili ya kuanza elimu ya darasa la kwanza huku
tukiamini ya kwamba atakuwa amesahau tukio lile lililompata,”alisema.
Amesema,
mtoto huyo alianza masomo yake na kuendelea vizuri mpaka juzi ambapo
walishangaa kumuona mtoto huyo akirudi nyumbani akiwa analia tena akitembea kwa
shida sana na ndipo walipombana na kumuuliza na kudai ya kwamba kijana yule
aliyemfanyia ukatili mwaka jana amemfanyia tena.
“Kwa kweli
tulishangaa kumuona mtoto akitembea tena kama kipindi cha awali na tulipombana
kwa kumuhoji ndipo alipotueleza ya kwamba kijana Daudi amemuingilia tena na
ndipo tulipochukua jukumu la kwenda kituo cha polisi”alisema.
Amesema,
kwakua mtoto alikuwa amechafuliwa sana iliwabidi wamsafishe pasipo fikiria ya
kwamba kitendo hicho kingepoteza ushahidi wenye nguvu.
Amesema,
walifika kwenye kituo cha polisi na kuchukua PF3 ambayo ingemuwezesha mtoto
huyo kutibiwa na kwenda nayo hospitali ya Rufaa ya Mbeya kitengo
cha huduma ya haraka ambapo walimkuta daktari na kuwaeleza ya kwamba masaa 72
yalikuwa yameshapita tokea tukio lifanyike hivyo yeye binafsi hana msaada
wowote ule.
“Mimi
nilishangaa sana kusikia kauli hii kwani ni kweli masaa hayo yalikuwa yamepita
lakini mbona hakumchunguza mtoto kwani kwa uwelewa wangu mdogo nikiangalia
sehemu za siri za haja kubwa za mtoto naona njia iko wazi,”alihoji Shangazi
huyo.
Ameongeza,
kuwa baada ya kuchoshwa na mizunguko isiyokuwa na matumaini iliwalazimu
kurudi nyumbani bila ya mtoto kufanyiwa uchunguzi mpaka siku ya pili
waliporudi, tena kwa msaada wa wanasheria na ndipo mtoto kufanyiwa uchunguzi na
kubainika ya kwamba njia ya haja kubwa ilikuwa imeharibiwa na sehemu ya
haja ndogo ilikuwa na uvimbe.
Amesema,
baada ya mtoto kupatiwa matibabu walirudi nyumbani na kuanza kuweka mitego ya
kumbaini muhusika na kufanikiwa kumkamata na kumfikisha kwenye
vyombo vya sheria polisi.
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Itiji, Leonard Magoma alikiri kupokea taarifa za tukio hilo
na kwamba serikali itasimamia suala hilo ili haki itendeke.
Hata hivyo
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba mtuhumiwa amekamatwa, upelelezi unafanyika mara
utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Mwisho.
Post a Comment