Haya ndio maajabu ya
Jiwe la Mbuji Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma
Maana ya neno Mbuji
ni "Kitu kikubwa"
1. Ni jiwe pekee
kubwa Mkoani Ruvuma,
2. lina vyanzo vingi
vya maji chini yake,
3. Ni ngumu kulipanda
na ukithubutu yatakayokukuta ni
juu yako na tayari Mzungu mmoja
kapoteza maisha'
4. Ni ngumu kulizunguka,
5. Hutumika kwa matambiko kwa baadhi ya
koo,
6. Kuna watu maalumu wanaotoa maelekezo
kwa yeyote
anayetaka kulifikia ama kupanda,
7. Ni kivutio kikubwa kwa wageni
wachache ambao
hutembelea Litembo, Maguu, Hagati nk
huko Mbinga,
8. Linaheshimika sana na wakazi
wanaolizunguka jiwe
hilo,
9. Sehemu kubwa ya
watu wananchi wanaolizunguka
hawajawahi kulipanda
wala kulisogelea kwa hofu,
10. Jina la jiwe hilo
ndilo jina la Tarafa ya Mbuji wilayani.Chanzo Maliasili zetu
Post a Comment