Kamanda wa polisi mbeya Ahmed Msangi |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
KIKONGWE wa miaka (71) ameripotiwa kupoteza maisha baada
ya kubakwa na mtu au watu wasiojulikana kisha mwili wake kutupwa shambani.
Tukio hilo lakusikitisha limetokea Mei 05 mwaka huu
majira ya saa 06:00 asubuhi huko katika kijiji cha Sisitila, Kata ya Sisitila,
Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya.
Akithibitsha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa wa Polisi
Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi , amemtaja
marehemu huyo kuwa ni Mesia Shoti (71) Mkazi wa Kijiji cha Sisitila
Aidha, Msangi amsema kuwa baada ya polisi kuufanyia uchunguzi
mwili huo umekutwa na jeraha sehemu za
kichwani.
Amesema, Chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa na kwamba wili wa marehemu umehifadhiwa
hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Hata hivyo,Kamanda Msangi, amewaomba wakazi wa Mkoa wa Mbeya kutoa taarifa za mtu/watu waliohusika na tukio hilo
ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Mwisho.
Post a Comment