Miili ya wanafunzi hao ikipokelewa na wanafunzi wa chuo hicho cha mzumbe Campus ya Mbeya kwa ajili ya kuagwa chuoni hapo na kusafirishwa kwa ajili ya mazishi mkoani Tanga na Dar es salaam. |
Mhadhili wa Chuo hicho ambaye ndiye mwalimu wa darasa kwa marehemu hao Ndugu Lusekero akitoa neno la shukrani kwa wanachuo pamoja na viongozi mbalimbali namna walivyo shiriki katika msiba huo |
Mmoja wa Wahadhiri wa Chuo Cha Mzumbe Mwanasheria na wakili Steven John akiwa katika majonzi ya kupotelwa na wanafunzi wake. |
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Campus ya Mbeya Prof.Ernest Kihanga akiwa ameinama kwa majonzi makubwa hali iliyofanya ashindwe kutoa neno juu ya msiba huo. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
WANAFUNZI hao wawili wa Chuo cha Mzumbe Campus ya Mbeya, walipoteza maisha baada ya kuzama kwenye bwawa la maji la kunyweshea wanyama lililopo kwenye hifadhi ndogo ya Bonde la Ifisi Wilayani Mbeya.
Bwawa hilo linamilikiwa na Kanisa la
Kiinjili la Uinjilist lililopo eneo la Mbalizi, limetengenezwa kwa ajili
ya matumizi maalum ya kuhifadhi maji ili kutumika nyakati za kiangazi kwa ajili
ya wanyama ambao wamehifadhiwa kwenye bonde hilo kwa ajili ya shughuli
mbalimbali za kiutalii.
Awali akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa
Chuo cha Mzumbe Campus ya Mbeya, Profesa Ernest Kihanga, alisema uongozi
ulipata taarifa ya vifo hivyo majira ya saa kumi jioni Mei 2 mwaka huu .
Amesema kwamba wanafunzi wawili ambao ni
Maiko Tarime na Albart Shenkalwa wote wamezaliwa katika miaka ya 1991 na
1992.
Amesema, Marehemu Maiko anaishi
Mkoani Tabora huku marehemu Albart ni mkazi wa Tanga ambao wote kwa pamoja
wanatarajiwa kusafirishwa leo(jana) kuelekea nyumbani kwao kwa ajili ya maziko.
Akielezea tukio hilo, Kihanga
amesema wanafunzi hao ambao inasemekana walikuwa 14 wanaume kwa wanawake
waliongozana kwa pamoja na kwenda kwenye hifadhi hiyo kwa ajili ya kuangalia
wanyama mara baada ya chuo hicho kufungwa kwa muda wa wiki moja.
Amesema, imeelezwa kwamba baada ya
wanafunzi hao kuingia kwenye bwawa hilo la maji wakitumia Mitumbwi na Boti
zilizokuwa pembeni ndipo boti ilipinduka na marehemu Maiko kuanza kuzama.
Hata hivyo zoezi la kuwaaga marehemu hao limekwisha fanyika chuoni hapo ambapo teyari miili hiyo imekwisha safirishwa kwa ajili ya mazishi kwa mkoa wa Tanga na Dar es salaam.
mwisho
Hata hivyo zoezi la kuwaaga marehemu hao limekwisha fanyika chuoni hapo ambapo teyari miili hiyo imekwisha safirishwa kwa ajili ya mazishi kwa mkoa wa Tanga na Dar es salaam.
mwisho
Post a Comment