MPAMBANO wa kirafiki wa kimataifa kati ya Timu ya soka ya
Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) uliochezwa juzi Jijini hapa, umeingiza
kiasi cha shilingi milioni 31, 200,000.
Akizungumza na waandishi wa habari,Mwakilishi wa shirikisho
la soka nchini (TFF) kwa mikoa ya nyanda za juu kusini, Ayoub Nyenza, amesema
kuwa kiasi hicho cha fedha kimetokana na watazamaji 6,240.
Amesema kuwa katika mgao huo, shirikisho la soka nchini TFF
na lile la Afrka (CAF) zilipata kiasi cha shilingi milioni 15,236,440, wakati gharama za tiketi ni shilingi milioni
3,000,000.
Akifafanua zaidi amesema, kiasi cha shilingi cha sh. milioni 4,759,322 kilichukuliwa na
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) kama kodi ya ongezeko la dhamani (VAT).
Aidha, Nyenza amesema katika mchanganuo huo, gharama za
mchezo zimechukua kiasi cha shilingi milioni 4,668,135, huku wamiliki wa uwanja
Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiambulia shilingi milioni 3,516,101.
Post a Comment