Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi



 Na Emanuel Madafa,Mbeya
Jeshi la polisi mkoa wa mbeya kwa kushirikiana na askari wa nakonde nchini zambia linamshikilia jambazi mmoja aliyefahamika kwa jina la jimmy nyilenda raia wa zambia baada ya  kujeruhiwa kwa kupigwa risasi katika jaribio la unyang’anyi.

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 02.06.2014 majira ya saa 17:45 jioni katika eneo la mpakani kati ya tanzania na zambia [tunduma/nakonde].

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema kuwa  watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walifyatua risasi ovyo kwa lengo la kuwapora pesa wabadilishaji fedha wa eneo hilo na polisi wa tunduma [tanzania] na nakonde [zambia] walikabiliana na majambazi hao.
 Katika majibizano hayo, majambazi watatu waliuawa wawili  wakifahamika kuwa ni sikapwite boniphace  mfanyakazi wa council nakonde raia wa zambia na chapwa kipakwa raia na mkazi wa zambia  na mwingine hakuweza kufahamika.

Aidha majambazi wengine waliweza kukimbia na jambazi mmoja jimmy nyilenda raia wa zambia amekamatwa akiwa  mahututi baada ya  kujeruhiwa kwa kupigwa risasi.

Katika tukio hilo silaha mbili aina ya ak-47 zenye namba 625562 na 1963ec58 zilikamatwa. Hata hivyo katika majibizano hayo raia wawili wa nakonde –zambia walijeruhiwa na wamelazwa kituo cha afya tunduma.hakuna madhara kwa askari na silaha zipo polisi nakonde zambia huku Juhudi za kuwatafuta majambazi waliokimbia zinaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. Msangi anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali walipo watuhumiwa hao wa tukio la ujambazi azitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Aidha anatoa wito kwa wafanyabiashara kuwa makini kwa kuchukua tahadhari katika kazi zao.
MWISHO

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top