MAKAMU wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema dawa za kulevya
ni tishio, kwa kuwa zinapunguza na kudhorotesha kasi ya maendeleo ya
nchi.
Kadhalika, amesema wimbi la vijana wengi kukamatwa na kufunghwa
nje ya nchi kutokana na kujihusisha na vitendo vya biashara haramu ya dawa za
kulevya vinaleta taswira mbaya na kulitia aibu taifa.
Aliyasema hayo jana Jijini hapa, wakati wa maadhimisho ya siku ya
kupinga vita dawa za kulevya duniani, ambapo kitaifa yalifanyika mkoani Mbeya.
Akihutubia umati wa wananchi katika katika uwanja wa Ruanda Nzovwe
Jijini hapa, Makamu wa Rais, Dk. Bilal alisema,dawa za kulevya ni tishio kwa
maendeleo ya taifa kwa sababu hupunguza nguvu kazi ya taifa.
Amesema matumizi ya dawa za kulevya huzorotesha afya za watumiaji
na huongeza vitendo vya uhalifu katika jamii, lakini pia
husababisha gharama nyingine zisizo za lazima kwa taifa.
Alisema vitendo vya watanzania, hususani vijana kujihusisha na
biashara ya kulevya ndani na nje ya nchi vimeendelea kwa kasi kubwa kutokana na
taarifa za kukamastwa kwao.
“Takwimu za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa kimataifa,
kuanzia mwaka 2006 hadi Aprili 2014 jumla ya watanzania 291 wanatumikia
vifungo mbalimbali katika nchi za China na Brazil baada ya
kuhukumiwa vifungo kwa makosa ya biashara haramu za dawa
za kulevya.” Alifafanua Dk. Bilal.
Aidha, ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2011
hadi Mei 2014 kulikuwa na jumla ya watumiaji 1526 wa dawa za kulevya waliokuwa
wakiendelea kupatiwa tiba kwa kutumia dawa Methadone katika hospitali ya Taifa
Muhimbili, Mwananyamala na Temeke.
Amesema kati ya watu hao waliobainika kutumia dawa hizo na
kuanzishiwa matibabu, wanaume walikuwa 1321, huku wanawake idadi yao ikiwa ni
205.
Alisema athari nyingine zinazotokana zinazxotokana na
matumizi ya dawa za kulevya ni kuongezekas kwa maambukizi ya virus vya Ukimwi
kutokana na waathirika kufanya ngono uzembe.
Dk. Bilal alisema kuwa, kutokanma na hali serikali imeendelea na
jitihadfa za kupambana na tatizo hilo ambapo Januari 2009 hadi Mei 20014 jumla
ya watuhumiwa 13,846 walikamatwa kwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.
Amesema
watu hao walikamtwa wakiwa na aina tofauti tofauti za dawa hizo ambazo ni
Heroin kilo 966.06, Kokeini kilo 363.7,wakati dawa aina ya Mirungi kilo 45,734,
huku bangi ikiwa ni tani 212.071.
Vile vile amesema, vikosi kazi vya kimataifa vya kupambana na
uhalifu katika bahari ya Hindi vinavyopambana na dawa za kulevya na uharamia
vijulikanavyo kama (Combained Task Force-150) vilifanikiwa kukamata jumla ya
kilo 2300 za dawa za kulevya aina ya Heroin kuanzia januari hadi Mei 2014.
Dk.
Bilali amesema dawa hizo zilikusudiwa kuingizwa katika ukanda wa
pwani wa Afrika Mashariki zikiswemo Tanzania, Kenya na Somalia.
Katika hali nyingine, Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri Mkuu sera
uratibu na Bunge, Wiliam Lukuvu, akimkaribisha mgeni rasmi katioka maadhimisho hahyo,
alisema kati ya vijana zaidi ya 400 waliokamatwa katika nchi mbalimbali duniani
wanahatari ya kuishia kunyongwa.
Katika maadhimisho hayo, Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya,
Rehema Chalamila, aliibua simanzi kubwa kwa wananchi waliohudhuria maadhimisho
hayo baada ya kutoa ushuhuda wake wa namna alivyoweza kujiingiza kwenye
utumiaji wa dawa hizo na madhara aliyoyapata kwake na familia yake.
Mwisho.






Post a Comment