Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Afisa Uhamiaji Mkoa Mbeya Asumso Achecha akizUngumza na wandishi wa habari Mkoani mbeya kuhusiana na ukamati wa wahamiji haramu nchini kupitia mkoa wa mbeya ambapo katika taarifa yake amedai kuwa sheria ya kuwabana mawakala wa wahamiaji harabu bado haitoshi.
Baadhi ya wahamiaji haramu kutoaka Nchini Kongo na Burundi ambao wamekamatwa na maofisa wa uhamijia Mkoani Mbeya ambao wamekamtiwa Tunduma Wilayani Momba wakielekea Nchini Malawi.
Mmoja wa wahamiji hao kutoka Mkoa wa Sidikifu  Nchini Burundi Ndugu Chekabitu Byawombi akielezea namna walivyosafirishwa kutoka nchini mwao hadi hatua ya kukamatwa kwao Nchini Tanzania.

Na EmanuelMadafa,Mbeya
DARA ya Uhamiaji Mkoani Mbeya imekili kuwa adhabu inayotolewa kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya kuingiza wahamijai haramu nchini ni ndogo na haiwezi kukomesha vitendo hivyo .
 
Hatua inakuja kufuatia kuwepo kwa ongezeko la Idadi kubwa ya wahamiaji haramu wanaoingia Nchini Kupitia Mipaka ya Tanzania na Malawi pamoja na Zambia.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisi Kwake Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya Ndugu Asumso Achecha amesema sheria inayotumika sasa bado inatoa mianya ya baadhi ya watanzania kuendelea kujihusisha na biashara hiyo haramu.
 
Amesema sheria inayotumika kwa sasa ni ile ya mwaka   1995  ambayo imekuwa ikitoa adhabu ya faini ya shilingi laki Moja au jela mwaka mmoja kitendo ambacho hakizuii tatizo badala yake inaongeza tatizo kweni wengi wao wamekuwa wakilipa faini na kuachiwa huru.
 
Amesema kutokana na hali hiyo Idara ya Uhamiaji ipo katika mchakato wa kufanya maboresho  hususani katika kipengele hicho cha sheria .
 
Hata hivyo amebainisha kuwa lengo la kutoa adhabu hiyo ni kuzuia au kupunguza kabisa tatizo hilo lakini mpaka mpaka sasa vitendo hivyo vimekuwa vikiendelea hasa kwa kuhusisha watanzania
 
Aidha Afisa Uhamiaji huyo amesema kuwa mpaka sasa  jumla wahamiaji haramu  266  wamekamatwa mkoani mbeya kwa kosa la kuingia nchini bila wakiwemo watanzania watatu kwa kuanzia mwezi January hadi mwezi June.
 
Katika  idadi hiyo  nchi ya Ethiopia  imetajwa kuwa na idadi kubwa  ya wahamiaji waliokamatwa kutokana kuingia nchini bila kibali ambao ni 205 huku wakongo wakiwa  32 pamoja warundi 22.
 
Wengine  wanne  kutoka Somalia  pamoja na Wamalawi wawili  na Mkenya  Mmoja ambao wote kwa ujumla wake walifikishwa  mahakamani na kupewa adhabu mbalimbali ikiwemo vifungo.
 
Hata hivyo Afisa uhamiaji huyo amebainisha sababu za  wahamiaji hao  kuingia nchini bila  husuani kwa mkoa huo ambao   unatokana na mkoa wa mbeya  kuunganisha Tanzania na nchi za  kusini mwa afrika.
 
Amesema kutokana na hali hiyo watu hao wamekuwa wakitumia njia hiyo kupita kwenda Afrika kusini na baadaye  kwenda nchi za Ulaya na wengine kubaki nchini hali ambayo imekuwa ikichangia kuongezeka kwa vitendo vya ugaidi pamoja na usambazaji wa madawa ya kulevya .
 
Kufuatia hali hiyo Asumso  ametoa wito kwa wananchi  mkoani kuhakikisha wanatoa taarifa za uwepo wa watu wasio wafaham pamoja na kuacha tabia  ya kuwahifadhi watu haon kwa maslahi ya Taifa.
Asumso Achacha ameendelea   kuwashukuru wananchi kwa ushirikano wanaoutoa kwa idara hiyo katika kuwabaini watu hao..
mwisho

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top