| Mchungaji mwasumbi mwenye koti jeupe |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Mahakama Kuu Kanda ya
Mbeya, imebatilisha hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12
aliyokuwa akiitumikia Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya,
Daniel Mwasumbi(57) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya ubakaji na kumpa mimba
mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Itende Neema Beni(19) jijini hapa.
Mchungaji Mwasumbi alihukumiwa kifungo hicho, Januari 2 mwaka huu
na mahakama ya Wilaya ya Mbeya na Hakimu Gilbert Ndeuruo na Serikali
kuwakilishwa na wakili Achiles Mulisa, ambapo Mahakama ilimtia hatiani
Mchungaji katika makosa kinyume cha sheria kifungu cha 130(2)e na 131(1) sura
ya 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Awali Mchungaji Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wa kujitegemea Victor Mkumbe ambapo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 2008 hadi 2011 ambapo alimpa ujauzito na kumzalisha mwanafunzi huyo watoto wawili wa kiume kwa nyakati tofauti hivyo kumkatisha masomo kinyume cha sheria.
Katika Rufaa hiyo Mchungaji Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wakujitegemea Benjamin Mwakagamba kutoka Dar es Salaam wakati Serikali iliwakilishwa na Wakili Prosister Paul.
Awali Mchungaji Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wa kujitegemea Victor Mkumbe ambapo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 2008 hadi 2011 ambapo alimpa ujauzito na kumzalisha mwanafunzi huyo watoto wawili wa kiume kwa nyakati tofauti hivyo kumkatisha masomo kinyume cha sheria.
Katika Rufaa hiyo Mchungaji Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wakujitegemea Benjamin Mwakagamba kutoka Dar es Salaam wakati Serikali iliwakilishwa na Wakili Prosister Paul.
Akisoma hukumu ya rufaa hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya,
Atuganile Ngwala, alisema kuwa sababu zilizowasilishwa kwenye
mahakama hiyo na Wakili wa upande wa utetezi zilidhihirisha kuwa kulikuwa
na ukiukwaji wa kisheria kwenye hukumu hiyo.
Jaji Ngwala ambaye alitumia takribani saa 1:15 kusoma huku hiyo
alisema katika utoaji wa hukumu hiyo haukuzingatia vipengele muhimu vya
kisheria viilivyotumika na mahakama ya wilaya kumtia hatiani Mchungaji
Mwasumbi.
Ameongeza kwamba kama ilivyoelezwa na wakili Mwakagamba,
muda wa lilitopotekea tukio hilo na liliporitiwa kwenye vyombo vya
usalama unaonekana kuchelewa na kukinzana, lakini pia ushahidi ulitolewa
mahakamani hapo na Mhanga ulionekana kujichanganya hivyo haujaonesha mrufani
kutenda kosa hilo’.
Awali Jaji Ngwala alimwita mchungaji Mwasumbi kuwa ni mende, na ni
mtu hatari sana katika jamii kwa kosa kama hilo na hafai kuwa katika jamii
jambo lililowafanya watu waliokuwa wakifuatilia mwenendo wa hukumu hiyo kuanza
kuinamisha vichwa chini akiwemo Katibu wa Kanisa la Uinjisti Bwana Mwakasole.
Lakini baadaye, Jaji Ngwala alionesha hisia zake kwamba
kutokana na kujichanganya kwa ushihidi hususani wa shahidi namba moja ambaye ni
binti aliyefanyiwa kitendo hicho hivyo kumtoa hivyo na haonekani kama ana kosa.
Hata hivyo, Jaji Ngwala alisema kuwa kwa upande wa Jamhuri ambao
ulikuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali, Prosister Paul una haki zote za
kukata rufaa na kesi kuanza upya endapo utaona haujaridhika na hukumu hiyo.
Wakili aliyekuwa akimtetea Mchungaji Mwasumbi amesema kuwa katika
rufaa ya mteja wake aliwasilisha sababu saba za kupinga hukumu hiyo ambapo
alidai kuwa hakimu wakati wa kutoa hukumu hiyo alikosea kisheria na haki
muda wa kuripotiwa kwa shauri hilo kwa vyombo vya usalama na lilipotokea
ulikinzana na kwamba aliegemea kwa ushahidi wa Mhanga tu.
Sababu zingine alidai kuwa hakimu aliegemea katika ushahidi
au vidhibiti ambavyo awali alivikata mwenyewe, pia alidai kuwa hakimu
hakuangalia uhalisia kosa lenyewe na badala yake alionekana kutoa maoni yake
binafsi.
Lakini sababu nyingine wakili Mwakagamba alisema kuwa hakimu huyo,
aliegemea ushahidi ambao ulijichanganya, wendesha mashtaka walishindwa
kuwapeleka mahakamani hapo mashahidi wa msingi katika kesi hiyo, hakimu
aliegemea upande wa vyeti vya watoto wawil waliodaiwa ni wa Mchungaji Mwasumbi
ambapo vyeti vilidurufiwa (photocopy) na si vyeti halisi na mwisho hakimu
huyo alitoa hukumu ambayo haikufuata mtiririko uliosahihi wa mashahidi husika.
Hata hivyo nje ya Mahakama ndugu na jamaa waliofurika kusikiliza hatma ya Rufaa hiyo waliokuwa na hamu ya kumlaki kwa furaha Mchungaji Mwasimbi ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kushindwa kutokana na Maafisa wa Magereza kumpeleka Gerza la Ruanda kukamilisha taratibu za Magereza.
Mwisho






Post a Comment