![]() |
| Miss Mbeya 2014 Atukuzwe Fabian akiwa na washindi wengine |
![]() |
| Miss Mbeya 2014 akikabidhiwa zawadi yake |
![]() |
| Wazee wa Ngwasuma kama kawaida yao |
![]() |
| Timu ya majaji kabla ya kumtangaza mshindi. |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Kinyanganyiro cha kumtafuta
mnyange wa mkoa wa Mbeya kwa mwaka 2014, kiliteguliwa usiku wa ijumaa baada ya
Mrembo Atukuzwe Fabian msomi wa chuo
kikuu kwa kuwabwaga warembo wengine 11
waliojitokeza.
Nyota ya mrembo huyo
ilianza kuonekana mapema, katika mavazi yote aliyovaa, lakini zaidi
aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa City Pub baada ya kujibu swali kwa ustadi lililouliza atamshauri
nini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abaas Kandoro endapo atapata fursa ya kukutana naye.
Mshindi wa Pili katika
shindano hilo ni Anitha Patrick Huku Matrida Hilu akishika
nafasi ya Tatu .
Washindi hao watawakilisha
mkoa wa Mbeya katika shindano la kanda
mwishoni mwa mwezi huu Mkoani Iringa .
Hata hivyo katika mtanange
huo Bendi Maarufu na Kongwe katika Nyanja za burudani toka jijini Dar es salaam
Fm Academia wazee wa ngwasuma wakiongozwa na Nyoshi,Patcho Mwamba na Baroteli
waliweza kuwapagawisha mashabiki na wapenda burudani walifurika katika viwanja
hivyo vya City Pub jijini Mbeya.
Pamoja na Burudani hiyo pia
wapenzi wa burudani waliohudhuria katika viwanja hivyo vya city Pub wamedai
kuwa shindano hilo limekuwa la kipekee hasa kutokana na kuwepo kjwa ulinzi wa
kutosha pamoja na hali ya hewa kuwa nzuri tofauti na mwaka jana.
MWISHO.




















Post a Comment