Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Dr. Mohamed Kiholile


 Na EmanuelMadafa,Mbeya
Jumla  ya  akina  mama  wajawazito  67,542  wameandikishwa na kulipiwa  jumla ya shilingi 699,156,000 kwa ajili ya mchango wa mfuko wa afya ya jamii CHF kwa  Mkoa wa mbeya.
Uandikishaji huo ni sehemu ya  mradi KFW  ambao  unalengo la kupunguza  vifo vya akina mama  kama ilivyo katika  mpango wa  maendeleo wa millenia namba 5  ili  kufikia malengo  mwaka 2015.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nhif  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Daktari Mohamed Kiholile amesema    utekelezaji wa  Chf kwa mkoa wa mbeya  umepata nguvu kubwa  kutokana na kuwepo kwa mradi wa  KFW .

Amesema  mradi huo unaendeshwa na mfuko wa taifa wa bima ya afya  ukishirikiana  na Benki ya maendeleo  ya watu wa ujerumani   ambapo lengo ni kuboresha  afya  ya akinamama  wajawazito  na watoto sanjali na kuimarisha  afya kwa ujumla.

Amefafanua kuwa zaidi ya shilingi  milioni 650  zimekwisha lipwa  kwenye Halmashauri fedha ambazo nii muhimu sana  katika kuboresha  huduma za afya  maeneo ya vijijini  na mijini.
Hata hivyo Meneja huyo ameelezea changamoto zilizopo katika mradi wa Kfw  ni pamoja na  mapungufu  ya utunzaji  takwimu  za kinamama wa Kfw walioandikishwa hasa kwenye ngazi  za vito  kama zahanati na vituo vya afya.

Changamoto nyingine ni suala la ugawaji wa  kadi za  CHF  kwa kinamama wa mradi  Kfw  waliokoma uanachama  wa NHIF  kuwa umekuwa wa kusuasua  na hauendani na kasi ya uandikishaji .
Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top