Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Bi.Mariam Ibrahim akiwa na mumewe



 Na EmanuelMadafa
Afisa mmoja mwandamizi katika wizara ya maswala ya kigeni nchini Sudan amesema kuwa mwanamke aliyepewa hukumu ya kifo kwa kubadili dini yake ya kiislamu,Meriam Ibrahim atawachiliwa huru katika kipindi cha siku chache zijazo.

Abdullahi Alzareg ambaye ni katibu katika wizara hiyo amesema kuwa Sudan inatilia maanani uhuru wa kuabudu na kwamba serikali itamtetea mwananmke huyo.

Kumekuwa na shutma za kimataifa kuhusu hukumu aliyopewa mwanamke huyo.

Meriam Ibrahim anazuiliwa katika jela moja ambapo alijifungua mtoto wa kike juma hili.

Ameolewa na mkristo na pia amehukumiwa kuchapwa viboko mia moja kwa kuzini kwa sababu mwanamke wa kiislamu kuolewa na mkristo ni haramu kulingana na sheria za Sudan.CHANZO BBC SWAHILI

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top