| Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmedi Msangi |
| Baadhi ya majeruhi wakiwa katika Hospital ya Ifisi Mbeya |
Watu Sita wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya
basi la Kampuni Ndejela Express lenye namba za usajili T 257 CMP aina ya TATA
likiendeshwa na Dereva wa kike Vailet Mbinda(31) mkazi wa Sokomatola kugongwa kwa nyuma na roli la mizigo kisha
kupinduka Kijiji cha Nanyala Kata ya Nanyala wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa tisa alasiri barabara ya
Tunduma/Mbeya ambapo roli lenye namba T
369 AWM aina ya SCANIA likendeshwa na Dereva asiyefahamika likiwa katika mwendo
kasi liligonga basi kwa nyuma kisha magari yote mawili kupinduka.
Miongoni mwa waliofariki ni Zainabu Mohammed aliyekuwa
kondakta wa basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Sumbawanga kila
siku, Padri Barnaba Lwemba 35 wa Morogoro Emmanuel Philipo 1 wa Sumbawanga
Neusta Jacob Mafuga 27 wa iringa Milika Mbingamno 38
Mwanaume mmoja na Mwanamke mmoja walifariki eneo la tukio na
wawili walifariki wakati wakipatiwa
matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya wakati majeruhi wanane walikimbizwa
Rufaa kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na juhudi
za kumtafuta Dereva wa roli zinaendelea.
Aidha amewataka wamiliki wa magari na madereva kuyafanyia
matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara magari yao ili kuepusha ajali
zinazoweza kuepukika.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya ya MbeyaIfisi,
Sikitu Mbilinyi amewataja majeruhi kuwa ni Dereva amewataja majeruhi kuwa ni
Fred,Maiko Malema(16),Justin Komb(24),Amir Ramadhan(26),Nausi
Bakari(28),Jackson Kambo(19),Anoria Ndezi(13) na Lucy Edson(17).
Mbilinyi amewataja wengine kuwa ni Groly Paul(27),Moyo
Safi(1),Rahma Peter(3),Mary Kitine(57),Mariam,Karen Naiman,Mecy,Adelina
Malipesa(52),Suzana Athas(35),Adelina Essau(28),Frola Essau(64) na Emmy
Charles(21).
Wengine waliolazwa ni pamoja na Diana Jumbe(19),Esther
Seleman(21),Paul Mayeta(45)ambaye ni Dereva msaidizi,Bahati Julius(33) na Joeph
Komba(34).
Kwa mujibu wa Muuguzi Mkuu hali za majeruhi zinaendelea
vizuri na wanafanya kilajitihada za kuokoa maisha yao na kutoa wito kwa
wananchi kujitokeza kuchangia damu kwani Hospitali hiyo ina uhitaji mkubwa
kutokana na kuwa karibu ya barabara kuu na ajali zinazojitokeza mara kwa mara
ingawa hupatiwa damu kutoka Benki ya Damu salama.
Hata hivyo baadhi ya abiria wamelalamikia kitendo cha baadhi
ya wananchi wa Nanyala badala ya kusaidia majeruhi walikuwa wakiwapora
mizigo,simu na fedha pia waliokuwa na vito vya thamani kama heleni.Picha story Mbeya yetu
mwisho.






Post a Comment