Mumewe mwanamke aliyehukumiwa kifo
nchini Suudan kwa kosa la kuasi dini ya kiisilamu, ameambia BBC kuwa
hajafahamishwa kuhusu mpango wa kumwachilia mkewe.
Ripoti zilizotolewa Jumamosi
ziliarifu kwamba afisa mmoja wa serikali alithibitisha Meriam Ibrahim,
aliyejifungua mtoto akiwa kizuizini ataachiliwa katika siku chache zijazo.
Lakini wizara ya mambo ya nchi hiyo
imesema kuwa Bi Ibrahim anaweza tu kuachiliwa ikiwa kesi yake ya rufaa
itafanikiwa.
Taarifa za hukumu ya kifo
iliyotolewa kwa mwanamke huyo, zimeikera sana jamii ya kimataifa.
Bi Ibrahim, alilelewa na mama aliyekuwa mkristo , lakini mahakama ilimhukumu
kifo ikisema kuwa anapaswa kuwa muisilamu, hiyo ndiyo iliyokuwa dini ya babake.
Alikataa kusilimu na kusema kuwa yeye ni mkristo na hivyo anakabiliwa na
hukumu ya kunyongwa kwa kosa la kuasi dini.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Abdullahi al-Azreg, aliambia BBC
Jumamosi kwamba, Bi Ibahim ataachiliwa huru kwani serikali ya Sudan inawapa
watu uhuru wa kuabudu na hivyo iko tayari kumlinda.
Mumewe Meriam Daniel Wami, alisema kuwa taarifa za mkewe kuachiliwa ambazo
amezisikia kupitia vyombo vya habari, ni kama uvumi tu.
“Hakuna afisaa yeyote wa serikali amewasiliana name. Labda kuna mashauriano
kati ya serikali na maafisa wa kigeni , ikiwa ni hivyo taarifa hizo mimi
sina,’’ alisema Daniel.
“Mimi nitasubiri tu kesi ya rufaa ambayo mawakili wamewasilisha, na
ninatamai kuwa mke wangu ataachiliwa.’’
Waziri wa mambo ya nje alifafanua kuwa Bi Meriam anaweza tu kuwa huru ikiwa
mahakama itaamua hivyo katika kesi yake ya rufaa.CHANZO BBC SWAHILI







Post a Comment