![]() |
| Waziri wa viwanda na Biashara Dr Abdallah Kigoda |
Na Asengar Oscar, Tanga
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dr.Abdallah Kigoda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya kirafiki kati ya timu ya vijana ya Coastal Union na Handeni City utakaochezwa Jumamosi wiki hii wilayani humo.
Mchezo huo ni moja kati
ya mechi mbalimbali za majaribio wanazocheza timu hiyo lengo likiwa ni kukipa
makali kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya vijana ikiwemo Rolling Stone na
mengine yatakayojitokeza.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Salim
Bawazir amesema mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa soka Kigoda ambao awali
ulikuwa ukiitwa Azimio kuanzia majira ya saa kumi jioni.
Bawaziri timu hiyo
itaondoka wilaya ya Tanga Jumamosi asubuhi ili kuweza kufika mapema wilayani
humo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mechi hiyo ikiwemo kuwataka wapenzi wa
soka kujitokeza kwa wingi.
“Mchezo huu ni muhimu sana kwa timu
yetu ya vijana kwani wanajiandaa na mashandano mbalimbali hasa yale ya vijana
ikiwemo Rolling Stone na Kombe la Uhai Cup “Alisema Bawaziri .
Katika hatua nyengine
wachezaji wa waliosajiliwa kwenye timu ya Coastal Union ambayo inashiriki
mashindano ya ligi kuu Tanzania bara wanatarajiwa kuwasili mkoani Tanga muda
wowote kuanzia jana.
Mwisho.








Post a Comment