Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro akizungumza katika ufunguzi wa barabara mpya kutoka eneo la Meta hadi Stendi kuu ya Mabasi jijini Mbeya yenye urefu wa kilomita 2.

Mkuu wa Mkoa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi  wa barabara  akiwa pamoja na Meya wa jiji la Mbeya Athanus Kapunga  wa kwanza kushoto pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigalla wa Pili kushoto na  Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Daktari Samuel Lazaro wa kwanza kulia
Kandoro pamoja Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigalla wakifurahi kwa ishala ya kupiga makofi mara baada ya kuzindua barabara ya Meta Stendi Kuu (Mbalizi Road) yenye urefu wa kilomita 2.1 .Picha na Keneth Ngelesi


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro akipongezana na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigalla mara baada ya ukamilishaji wa zoezi la uzinduzi wa barabara hiyo

Mkuu wa Mkoa akipeana Mkono wa pongezi na Mkurugenzi wa miradi wa Kampuni ya CICO Ndugu Meng Yuan kampuni ambayo imejenga barabara hiyo.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya wakiwa katika eneo la Uzinduzi wa barabara hiyo
Baadhi ya madiwani hao wakiwa eneo la tukio

Mzee sefu na kikundi chake cha ngoma naye hakuwa mbali kutumbuiza 


Na EmanuelMadafa,Mbeya
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro  amewataka watumiaji wa barabara kutogeuza mifereji ya maji  machafu ambayo ipo kando ya barabara kama madampo ya kutupa taka badala yake wawe na  moyo wa  uchungu wa kutunza mifereji hiyo kutokana na kugharimu fedha nyingi.
 
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa kauli hiyo leo jijini Mbeya  wakati wa uzinduzi wa barabara ya Meta Stendi kuu yenye urefu wa kilometa 2.1  ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami.
 
Amesema kumeibuka kwa isiyo ya kistaarabu miongoni mwa wakazi wa jiji la Mbeya sanjali na  watumiaji wa barabara kuamua kugeuza mifereji hiyo kama sehemu ya kutupa taka wakati kuna madampo maalumu ambayo yametengwa kwa ajili ya utupaji wa taka.
 
Kandoro amefafanua kuwa  imekuwa ni kawaida kwa watumiaji wa barabara kuona kuwa mifereji hiyo iliyopo pembezoni mwa barabara ni sehemu ya kuhifadhi takataka na hivyo mji kuonekana ukiwa mchafu kutokana na tabia iliyojengeka ya kugeuza miferji hiyo ya kupitisha maji kama madampo.
 
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema  kuwa kila mtumiaji wa barabara anawajibu wa kutumia barabara vizuri bila kufanya uharibifu wa aina yeyote na kuzingatia kuwa serikali imetumia fedha nyingi kujenga barabara.
 
 Wakati huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa wito kwa viongozi wa jiji la Mbeya kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika suala la usimamizi wa usafi kw akuhakikisha kuwa taka zote zilizopo mitaani zinatolewa na kupelekwa katika eneo husika.
 
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Mbeya ,Athanas Kapunga alisema kuwa kutokamilika mapema kwa barabara hiyo kulimfanya kuwekwa kitimoto mara kwa mara  katika vikao  vya kamati ya ushauri ya Mkoa,kamati ya ushauri ya Wilaya pamoja na vikao vya mabaraza ya madiwani .
 
Amesema kuwa barabara hiyo ilishindwa kukamilika mapema kutokana na baadhi ya maeneo  kubainika kuwa na chem chem  hivyo kupelekea uharibifu wa barabara wa mara kwa mara hivyo ilibidi wafike wataalamu kutoka chuo kikuu  cha sayansi na Teknolojia(Must) kuafutia agizo la bodi ya barabara ya Mkoa kufanya utafiti wa udongo na kupata jibu na ndipo barabara hiyo ilipoanza kutengenezwa.
 
Amesema sababu nyingine ni  udongo uliokuwepo awali kwenye tabaka la mwanzo la udongo haukuwa  na ubora wa kuhimili uzito wa magari.
 
Naye  Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Dkt.Samweli Lazaro amesema kuwa  ujenzi wa barabara hiyo umemalizika kwa mkataba wa grama ya sh. Bil.1,553,437,275.00 kutoka kwenye grama za awali ambayo ni Bil.1,490,343,275.00 kati ya fedha hizo kiasi  cha sh. Bil.853,437,275.00 ni fedha kutoka mfuko  wa barabara na kwamba barabara hiyo ina urefu wa kilometa 2.1 na upana wa mita 7.5.
 Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top