![]() |
| Askofu Mkuu akionyesha baadhii ya vyandurua hivyo mbele wa washiriki katika hafla hiyo |
![]() |
| Mwenyekiti wa Kamati ya Maandali ya shughuli za ugawaji wa Vyandarua hivyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti cha( MMRC) Dr.Leonard Maboko akizungumza katika hafla hiyo. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
KANISA la Tanzania
Assemblies of God(TAG), limetoa jumla ya vyandarua 8550 vikiwa na
thamani ya shilingi milioni 280 katika hospitali na vituo vya afya 117 kwa
mikoa mitatu ya Nyanda za juu kusini.
Sanjali na utoaji huo wa
vyandarua pia kanisa hilo linatalajia kutoa damu katika benki ya damu salama
Mkoani Mbeya ambapo zaidi ya wachungaji 800
wa kanisa hilo watahusika katika shughuli hiyo.
Akikabidhi msaada
huo leo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abassi, Askafu Mkuu
wa Kanisa hilo Dr. Barnabas Mtokambali, amesema utoaji msaada huo unaenda
sambamba na maadhimisho ya miaka 75 ya uanzishwaji wa kanisa hilo nchini
Tanzania mwaka 1939.
Amesema, TAG ni sehemu
ya jamii kwani linatambua ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa maralia hivyo
ni vema likaunga mkono juhudi za serikali katika kufikia malengo ya milenia
kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Amesema, ugonjwa wa maralia
umekuwa ukiligharimu Taifa kwa kupoteza watoto chini ya miaka mitano na
mama wajawazito hivyo pamoja na kanisa kutoa huduma ya kiroho imeona
ni vema ikachangia sehemu iliyotolewa na waumini wa dhehebu hilo katika kuokoa
kizazi hicho.
Amesema wanatambua kuwa suala la utoaji huo wa vyandurua hauwezi kupunguza kabisa tatizo lakini kwa kiasi hicho kutasidia kuokoa kwa kiwango kikubwa changamoto ya uhaba wa vyandarua.
Amesema, vyandarua
1300 vitapelekwa Mkoani Rukwa kwa ajili ya Hospitali 3 na vituo vya afya na
Zahanati zinazolaza wagonjwa 22 huku vyandarua
3100 vitasambazwa Mkoani Njombe kwa ajili ya Hospitali 11 na vituo vya afya 25.
Amesema, vyandarua 4150
vitabaki Mkoani Mbeya kwa ajili ya Hospitali 20 na vituo vya afya na Zahanati 36.
Amesema, vyandarua
vitakavyogawiwa Mkoani Mbeya vimo vyandarua 650 vya
hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambapo kati yake 500 ni kwa ajili ya
hospitali kuu na 150 ni kwa ajili ya hospitali ya wazazi ya Meta.
Aidha, amesema kuwa
idadi ya vyandarua vinavyogawiwa katika kila hospitali na Vituo vya afya kwa
mikoa yote mitatu imefanyiwa upembuzi wa idadi ya vitanda vilivyomo ndani ya
hospitali hizo na kwenye vituo vya afya.
Akipokea vyandarua
hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro amesema kitendo
kilichofanywa na kanisa hilo kimeidharirishia jamii ya kwamba fedha
zinazotolewa na waumini kama sadaka zinatekeleza agizo la mungu la kuyasaidia
makundi muhimu.
Hata hivyo Mkuu huyowa
Mkoa wa Mbeya ametumia fursa hiyo kulitaka kanisa hilo kuendelea kutoa wito wa
waumini na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanaachana na tabia ya kutumia madawa
ya kulevya aina ya banki pamoja na pombe
haramu.
mwisho














Post a Comment